HATIMAYE Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na aliyekuwa mume wa Josephine Mushumbusi( KWA SASA NI MCHUMBA WA DR. SLAA) , Maimbo baada ya kuiona rufaa hiyo haina msingi wowote kisheria
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akiwa na Josephine Mushumbusi
Hukumu hiyo ya rufaa ya madai ya ndoa Na.32/2012 ilitolewa leo na
Hakimu Aniseth Wambura ambapo alisema mahakama yake imefikia uamuzi huo
wa kuitupa rufaa hiyo kwasababu haina mantiki ya kisheria.
Hakimu Wambura alisema mahakama yake imekubalina na hukumu
iliyotolewa Aprili 2012 na Mahakama ya Mwanzo Sinza katika kesi ya madai
talaka iliyokuwa imefunguliwa na Mushumbusi anayetetewa na wakili wa
kujitegemea Philemon Mutakyamilwa dhidi ya Maimbo ambapo mahakama hiyo
ya chini ilitangaza kuwa hakukuwa na ndoa baina ya watu hao kwasababu
Maimbo alikuwa ni mzinzi, simwaminifu katika ndoa yake na alikuwa
akimtesa mkewe.
“Baada ya mahakama yangu kusikiliza hoja za mwomba rufaa na mjibu
rufaa ,mahakama hii imefikia uamuzi wa kukubali hoja za Mushumbisi kuwa
kwa tabia ile ya mbaya ya uzinzi na ukosefu wa uaminifu katika ndoa yake
hapakuwepo na ndoa baina yao hivyo mahakama inatangaza kuwa hukumu
ya mahakama ya Mwanzo Sinza ambayo iliivunja ndoa hiyo ilikuwa hukumu
sahihi “alisema hakimu Wambura.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kutolewa kwa
hukumu hiyo wakili Mutakyamilwa alisema amefurahishwa na hukumu hiyo
kwani mahakama imetenda haki kwasababu kesi hiyo ya madai ya talaka
ilikuwa na msukumo wa siasa chafu zilizokuwa na lengo chafu la
kumchafulia jina mteja wake(Mshumbusi) ambaye kwa sasa ni mzazi mwenzie
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad
Slaa.
KWA HIYO, KWA SASA DR. SLAA NA MPENZI WAKE W ANAWEZA KUOANA..!!!
No comments: