Kutoka Bungeni Mjini Dodoma LEO Muda Mfupi Kabla Spika Wa Bunge Anne Makinda Kuahirisha tena Bunge kutokana na vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa kauli ya
Serikali Bungeni kuhusu vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara.
Spika
wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akiahirisha Bunge kutokana na vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara
Naibu
Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Pereira Ame Silima (Katikati), Naibu
wa Viwanda na Biashara Mhe. Greygory Teu (kushoto) na mbunge wa Kilosa
Mhe. Mustafa Mkullo wakizungumza nje ya ukumbi wa Bunge.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Emmanuel Nchimbi (Kushoto) akizungumza
na mbunge wa Kinondoni Mhe. Iddi Azzan nje ya ukumbi wa Bunge mara baada
ya bunge kuahirishwa.
Waziri
wa Nchi ofis ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Merry Nagu
akiomba kutengua kanuni ya Bunge Na. 38 ili kuruhusu suala la vurugu
za Mtwara kujadiliwa Bungeni.
Waziri
Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Mhe. Jaji Frederick Werema pamoja na baadhi ya Mawaziri ndani ya
ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha Bunge .
Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na baadhi
ya Mawaziri na Wabunge ndani ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Spika wa
Bunge kuahirisha bunge
Wabunge
wa Viti Maalumu wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge baada ya Spika kuahirisha
Bunge. Kutoka kushoto ni Mhe. Lucy Owenya(CHADEMA), Katikati Mhe.
Mkiwa Kimwanga(CUF) na kulia ni Mhe. Dkt. Merry Mwanjelwa(CCM).
Kundi
la Waandishi wa Habari wanaoripoti habari za Bunge wakitoka ndani ya
ukumbi huo mara baada ya Spika wa Bunge kuahirisha kikao cha Bunge.
No comments: