Sheha wa Shehia ya Tomonda Wilaya ya Magharibi Zanzibar Mohammed Kidevu, mchezaji wa Zamani wa Timu ya KMKM , Yanga na Timu ya Taifa ya Zanzibar Kidevu Amwagiwa Tindikali na Watu Wasiojulikana
Sheha wa Shehia ya Tomonda Mohammed Kidevu akiwa katika wodi ya
Hospitali kuu ya Rufaa MnazoMmoja akipata matibabu ya majaraha ya kitu
kinachosadikiwa kwa Tindi Kali,akipata matibabu hayo katika hospitali
hiyo.
Sheha wa Shehia ya Tomonda Wilaya ya Magharibi Mohammed Kidevu,
mchezaji wa Zamani wa Timu ya KMKM , Yanga na Timu ya Taifa ya Zanzibar
Kidevu usiku wa kuamkilia leo amemwagiwa tingi kali na Watu
wasiojulikana akiwa katika maeneo ya kwakehuko Tomondo jana usiku,
akipatiwa matibabu katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja alikolazwa kwa
matibabu na uchunguzi zaidi wa kitaalamu katika Hospitali hiyo.
Sheha
Mohammed Omary Said aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa
katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu, Sheikh
Mohammed amepata maumivu makali sehemu za kifuwa na jicho kuumia
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo
kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio
na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua
aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.Sheha
huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba
yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba
hakuweza kumtambua.
No comments: