KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS:MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA UTOKOMEZAJI WA UGONJWA WA FISTULA, JIJINI DAR
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwasili katika eneo lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kufanyia shughuli za maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais Dkt Bilal, akimjulia hali mtoto mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baba wa mtoto, Elizabeth Nora kutoka Dodoma aliyelazwa katika Hospitali ya CCBRT, wakati Makamu alipofika hospitalini hapo jana Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Dokta wa Hospitali ya CCBRT, wakati
alipokuwa akitembelea katika wodi za wagonjwa waliolazwa katika
Hospitali hiyo, alipofika hospitalini hapo jana Mei 23, 2013 kwa ajili
ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa
Ugonjwa wa Fistula. Kulia ni Mtoto Boniface Patrick akiwa na Baba yake,
Patrick Luwao, Wakazi wa Dodoma, akiwa amelazwa baada ya kufanyiwa
upasuaji na kuongezewa sehemu ya mguu uliokuwa mfupi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Stellah Nzyemba, ambaye awali alikuwa mgonjwa na baada
ya kutibiwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT na kupona ameajiriwa ili
kuwasaidia wagonjwa wa Fistula. Makamu alifika hospitalini hapo jana
Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
Balozi
wa Ugonjwa wa Fistula, Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Mwana FA,
akisoma hotuba yake kuhusiana na kuzunguka katika baadhi ya mikoa na
kutoa ujumbe kwa wananchi na hasa kina mama kuhusu Ugonjwa huo.
Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose, akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya
Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula, yaliyofanyika jana Mei 23, 2013
Jijini Dar es Salaam.
Wasanii 21 walioungana na kuimba wimbo wa Kidole kimoja,wakitoa burudani jukwaa .Picha na mdau Mbwana Ramadhani
No comments: