Ads Top

Kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais IKULU:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Gharib Bilal Audhuria Sherehe Za Kusimikwa Askofu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Mchungaji Emannuel Joseph Makala

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Mchungaji Emmanuel Joseph Makala, baada ya kuwekwa wakfu.
 Maaskofu waliosheresha wakfu huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu mpya wa Kanisa la Kiinjili  la Kilutheri Tanzania (KKKT)  Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Mchungaji  Emannuel Joseph Makala, baada ya kuwekwa wakfu na kuzinduliwa kwa Dayosisi  hiyo katika Kanisa la Ebeneza  Shinyanga mjini jana Mei 5, 2013. Katikati  ni Askofu Mkuu KKKT Tanzania, Dkt Alex Malasusa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia waumini wa Dini ya Kikristo wakati wa ghafla ya kuwekwa wakfu Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Mchungaji Emmanuel Joseph Makala na kuzinduliwa kwa Dayosisi hiyo mpya  ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria iliyofanyika jana katika kanisa la Ebeneza  Shinyanga mjini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya viongozi wakati wa ibada maalum ya kuwekwa Wakfu Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria na kuzinduliwa rasmi Dayosisi hiyo katika kanisa la Ebeneza  Shinyanga mjini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa KKKT Tanzania baada ya kuwekwa Wakfu Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria na kuzinduliwa rasmi Dayosisi hiyo katika kanisa la Ebeneza  Shinyanga mjini.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.