Marehemu Albert Mangwair enzi za uhai wake.
Akiongea kupitia kipindi cha Amplifire cha Clouds FM, kutoka
mkoani Morogoro, mama mzazi wa msanii Albert Mangwair aliyefariki dunia
leo akiwa nchini Afrika Kusini, amesema kuwa mara ya mwisho kuwasiliana
na marehemu ilikuwa wiki mbili zilizopita ambapo Mangwair alimwambia
kuwa mzima na anaendelea vizuri na kwamba angerejea nchini Ijumaa
iliyopita. Aliongeza kuwa taarifa za kifo cha mwanaye amezipata jioni
hii kwa masikitiko. Wakati Mangwair anaelekea Afrika Kusini hakumuaga
mama yake japo akiwa huko alikuwa anawasiliana naye. Kuhusu taarifa za
mazishi mama Mangwair amesema bado anasubiri shemeji zake wafike ili
wapange. Mungu ampumzishe Mangwair mahali pema peponi. Amen!
TWEET YAKE YA MWISHO ALBERT MANGWAIR
MAMA NGWAIR: MWANANGU ALINIAHIDI KURUDI IJUMAA ILIYOPITA
Reviewed by
uhurutz
on
15:16
Rating:
5
No comments: