Ads Top

TASWIRA: YA MVUA ZINAZO ENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR ES SALAAM

Hapa ni eneo la millenium tower makumbusho, mvua kubwa ilioyensha usiku wa leo na leo asubuhi imepelekea kuwepo kwa maji mengi eneo hili hadi kupelekea magari yaendayo posta kupitia pakinng ya magari ya eneo hili au ya jengo hili la millenium tower  na kusababisha msongamano wa magari toka asubuhi hadi sasa, na hata mabar  ya pembezoni mwa sehemu hii na grosari zote zimelazimika kufunga kwa muda hata maduka kutokana na maji mengi kuingia sehemu zao za biashara. 
hii ni mara kwa mara mvua inapokuwa kubwa tatizo hili kutokea na hatari zaidi kwa njia ya kuelekea mwenge kutoka moroco kuna mtaro ambao umefunikwa na maji hivi nawaasa wenye magari wasitanue eneeo hilo kwa mitaro haionekani na ni mikubwa hivi madereva wawe makini sana wafikapo eneo hili.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.