Lionel Messi hangelizuia kichapo walichopewa Bercelona cha magoli matatu kwa yai na Bayern Munich ya Ujumani.
Wachezaji wa Bayern Munich
Haya ni kwa mujibu wa mchezaji mwingine wa Barcelona Gerard Pique.
Arjen
Robben na Thomas Mueller walifunga bao moja kila mmojan naye Pique
akijifunga mwenyewe na kuiwezesha Bayern kufuzu kwa fainali ya kuwania
kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa jumla ya magoli 7-0.
Pique amesema licha ya kuwa Messi ndiye mchezaji bora zaidi duniani kwa sasa, hilo halikuwa tatizo la kushindwa kwao.
Messi kutoka Argentina, ambaye amefunga magoli
54 baada ya kucheza mechi 45 msimu huu, alitarajiwa kucheza katika
kipindi cha pili kama mchezaji wa ziada hasa baada ya kufunga bao kwenye
mechi ya ligi kuu siku ya Jumamosi dhidi ya Althletics Bilbao.
Kocha wa Barcelona Tito Vilanova, amesema
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alipata jeraha la paja wakati wa
mechi yao siku ya Jumamosi na hivyo ingelikuwa hatari zaidi ikiwa
angelicheza mechi hiyo akiwa na maumivu.
No comments: