Uhusiano kati ya wafanyakazi na wamiliki wa migodi umedorora Wachimba migodi kumi wamejeruhiwa nchini Afrika Kusini baada ya walinzi kuwafyatulia risasi za mipira wafanyakazi wa migodini.
Msemaji wa kampuni ya Lanxess,
inayomiliki mgodi wa Chrome mine, alisema kuwa polisi waliwafyatua
risasi hizo kama njia ya kujilinda.
Uhusiano kati ya wafanyakazi na wamiliki wa
migodi umedorora hasa baada ya polisi kuwaua wafanyakazi 34 wa migodini
katika mgodi wa Marikana mwaka jana.
Wiki jana wafanyakazi katika kampuni ya Lonmin waligoma kwa siku mbili.
Wachimba mgodi wa Lanxess chrome, walifanya
mgomo ambao haukuwa umepangwa baada ya kutofautiana na waajiri wao
kuhusu marupurupu yao.
Inaarifiwa kuwa hali imetulia baada ya
kufyatuliwa riusasi za mipira katika mgodi wa Rustenburg Kaskazini mwa
Johannesburg, na kuwa hakuna yeyote miongoni mwa waliojeruhiwa yuko
katika hali mbaya.
KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA..>>>>>>>>>>
KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA..>>>>>>>>>>
No comments: