Vipodozi vyenye kemikali, dawa bandia zinavyowaua Watanzania
Wanawake zaidi ya 6milioni nchini huenda wakaugua saratani,
kuzaa watoto wenye mtindo wa ubongo au kupoteza maisha kutokana na
kukithiri kwa matumizi ya vipodozi vyenye kemikali hatari.
Utafiti wa Profesa Msaidizi wa Chuo Kikuu cha
Georgia, Atlanta, Marekani, Kelly Lewis wa kitengo cha Sosholojia,
kuhusu wanawake wanaotumia ‘mkorogo’ Tanzania umebainisha hayo.
Taarifa ya utafiti huo inaonyesha kuwa asilimia 30
ya wanawake, sawa na 6 milioni ya wanawake wote nchini ambao ni milioni
23, wanatumia vipodozi vyenye kemikali hatari, vyenye madini ya zebaki,
hydroquinone na maji ya betri.
Dk Lewis akishirikiana na timu ya Watanzania 20,
aliwahoji wanawake 420 katika Jiji la Dar es Salaam ambapo wengi
walikiri kujichubua kwa sababu ya dhana kuwa weupe ni uzuri, pamoja na
kuwaridhisha wenza wao wanaopenda wanawake weupe.
Utafiti huo wa Shahada ya Uzamivu ulifanyika kuanzia mwaka 2000 na kumalizika Mei 17, 2012.
Profesa Lewis anasema kuwa vipodozi hivyo hasa
vyenye madini ya zebaki, kwa kiasi kikubwa husababisha ugumba, saratani
na maradhi ya figo.
“Inatisha.
“Inatisha.
Wanawake hawatumii ‘mikorogo’ ya dukani pekee,
lakini pia wanatengeneza mikorogo ya kijadi kwa kuchanganya asidi ya
maji ya betri ya gari, dawa ya meno na sabuni ya unga,” anasema Dk
Kelly.Akizungumza kwa njia ya Barua Pepe, Profesa Lewis anasema kuwa
anatarajia kufanya kipindi kuhusu wanawake wanaotumia mikorogo Tanzania
ili kutoa elimu.
‘Kutokana na maombi mengi, nimefungua Kituo cha Utalii kwa Umma na nitafanya safari mbili za kuja nchini Tanzania,” anasema.
TFDA imebainisha vipodozi vyenye sumu kuwa ni
pamoja na ni Carolight, inayotajwa kuwa na sumu kali zaidi pamoja na
vile vyenye madini ya zebaki au mercury, ikiwamo sabuni ya Jaribu na
Mekako.
Vipodozi vingine ni vile vilivyochanganywa na
viambata sumu kama Clobetasol na Betamethasone ambapo itajwa pia krimu
ya Amira, Betasol na Skin Success.
Inaelezwa kuwa wanawake wanaotumia mafuta ya aina hiyo wakiwa wajawazito huwaathiri watoto walioko tumboni.
Asilimia 70 ya vipodozi hivyo hutoka nje ya nchi, ambapo imebainika kuwa hakuna sheria kali za udhibiti wa dawa na vipodozi.
No comments: