TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA


Mmoja wa majeruhi akifikishwa hospitali

Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea


Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea

Ulinzi umeimarishwa


Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa
habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi
mkali wa Polisi.


Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio

Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.


Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.

Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na
wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote
waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa.
Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika
eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa
tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa
Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.


Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu
kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya
waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao
wakiwa ni majeruhi.




Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa
mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani
hapo.








No comments: