Ads Top

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA: Spika wa Bunge Anna Makinda ameahirisha shughuli za Bunge Bunge baada ya kusomwa kwa hotuba ya Waziri Mkuu kuhusu ufafanuzi wa vurugu za kupinga kusafirishwa kwa gesi zilizotokea jana mkoani Mtwara

 
Waziri Nchimbi akisoma Hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu Bungeni leo
  Kabla ya kuahirishwa kwa Bunge hilo, kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa mambo ya Ndani Dk Emmanuel Nchimbi alisoma hotuba hiyo iliyolaani vikali kutokea kwa vurugu hizo.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa hatua ya Serikali kutaka kujenga bomba la gesi ni hatua zinazofanywa na mataifa mengi duniani, hivyo kundi linalochochea vurugu hizo litatafutwa nje na ndani ya Tanzania kwa namna yeyote.

Akiahirisha shughuli za Bunge Spika Makinda alisema, pamoja na kuwepo kwa wachangiaji wengi wa wizara ya hiyo anasitisha shughuli za Bunge ili kutoa nafasi kwa kamati yake ya uongozi kuchambua suala hilo kwa upana zaidi.

"kesho tutaendelea na ratiba kama kawaida ambapo Wizara ya Afrika Mashariki itasoma bajeti yake, Wizara hii ya nishati na madini tutaipangia muda mwingine ili iweze kumaliza mambo yake, naomba tuelewe kuwa wizara kama wizara haina tatizo lolote isipokuwa suala hili la gesi ya mtwara ndiyo imetufanya tuitafutie siku nyingine ya kumalizia kazi zao"alisema Spika Makinda

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.