Dar es Salaam. Idara ya Ujasusi ya Marekani imeweka bayana kwamba inajitegemea kwa ulinzi katika ziara nzima ya Rais Barack Obama kwa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senegal
Dar es Salaam. Idara ya Ujasusi ya Marekani imeweka bayana kwamba inajitegemea kwa ulinzi katika ziara nzima ya Rais Barack Obama kwa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senegal.
Kwa mujibu wa taarifa ya idara hiyo, katika
kuhakikisha usalama wa kutosha wakati wa ziara ya Obama tayari maofisa
wao wameshakamilisha maandalizi ya kiusalama katika nchi zote
anazotarajiwa kutembelea.
Meli ya kivita kutua bandarini
Katika kuchukua hatua hizo, meli kubwa kabisa ya
kivita yenye hospitali maalum zipo tayari kwa ya kambi maalumu katika
bandari maalum za nchi atakazotembelea, kwa ajili ya kukabiliana na
dharura yoyote ya kiafya ya Obama na familia yake.
Ili kuwawezesha maofisa wa kijasusi wa Marekani,
ndege ya kijeshi ndiyo itakayobeba magari 56 zikiwemo limousine 14 na
magari matatu maalumu ya kubeba mizigo.
Malori hayo yatakuwa yakibeba vioo ambavyo ni
vizuizi maalumu vya risasi na milipuko kwa ajili ya kuongeza ulinzi
kwenye hoteli atakazolala yeye na familia yake.
Ndege za kivita kutawala anga
Ndege za kivita zitakuwa zikiruka kwa zamu wakati
wote muda wa sasa 24 kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi katika sehemu
atakayokuwa Rais Obama na kudhibiti anga yote kwa wakati huo dhidi ya
ndege yoyote ngeni itakatosogea usawa wao.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mwananchi,
hakuna Maandalizi ya safari hiyo ambayo tayari yamekamilika
yanapolinganishwa na safari nyingine za aina hiyo zilizowahi kufanyika,
waraka maalumu kuhusu suala la usalama unaonesha kwamba kumekuwa na
juhudi za ziada zakuhakikisha ulinzi wa Amiri jeshi huyo Mkuu wa
Marekani akiwa nje ya nchi.
Kabla ya safari yake kwa nchi za Afrika, Obama
atatembelea Ireland na Ujerumani ikiwa ni sehemu ya kuongeza changamoto
inayokabili masuala ya usalama wake.
Lakini zaidi, safari ya Obama kwa nchi za Afrika
inadhaniwa kuwa inayolazimisha waandaaji kuwa na umakini wa hali ya juu
na kuifanya iwe aghali zaidi katika utawala wa Obama kuliko ziara katika
nchi za ulaya, kwa mujibu wa wataalamu wa mipango.
Familia ya rais huyo inatarajiwa kutembelea nchi
tatu za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senagal kuanzia Juni
26 hadi Julai 3 mwaka huu
Serikali ya Marekani inahakikisha kwamba inasimamia kwa silimia
100 ulinzi wa familia hiyo inapokuwa nje ya nchi na haihitaji kutumia
vyombo vya usalama vya nchi husika ikiwemo polisi, majeshi, na huduma za
hospitali.
Safari yaahirishwa
Katika ziara ya Obama nchini Tanzania, safari ya
kutembelea Mbuga ya Wanyama ya Mikumi yeye pamoja na familia yake
imeahirishwa ili kupunguza ukubwa wa gharama katika safari yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi, Obama
hatatembelea tena mbuga za wanyama kama ilivyopangwa awali, bali
imependekezwa kwamba sehemu atakayoweza kufika ni katika Gereza la
Visiwa vya Roben nchini Afrika Kusini ambako Rais wa zamani wa Afrika
Kusini, Nelson Mandela.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, kuahirishwa kwa safari
ya mbugani kunatokana na gharama kubwa inayohitajika kwa ajili ya
kupata walinzi maalumu wakiwemo wadunguaji wenye silaha nzito ambao
watakabiliana na wanyama wakali.
Safari hii ya Obama nje ya nchi zinafanyika wakati
wakala wa Serikali ikiwemo Idara Maalumu ya Ujasusi zikichuana kuhusu
namna ya kupunguza matumizi.
Idara hiyo inalazimika kupunguza kiasi cha Dola 84
milioni (Sh134.2 bilioni) mwaka huu na hiyo inailazimisha kufuta safari
ya kitalii ya Ikulu ya Marekani ambayo itasaidia kuokoa Dola 74,000
(Sh118.2 milioni ) kama posho ya muda wa ziada wa kazi kwa wiki kwa kila
askari.
Gharama za safari hii
Safari ya sasa ya Obama itagharimu serikali kuu
kati ya Dola 60 milioni hadi Dola 100 milioni (Sh 159.2 bilioni), kwa
makadirio ya safari za aina hiyo zilizofanyika kwa mataifa ya Afrika
miaka ya hivi karibuni.
Makadirio hayo yamefanywa na mmoja wa wataalamu
wenye uzoefu na safari hizo ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa
si msemaji rasmi.
No comments: