Habari zilizotapakaa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Johannesburg ni kwamba hakuna matumaini ya Mandela kupona na sasa familia yake inajadiliana kuhusu taratibu za mazishi yake huku mwenyewe akiendelea kupumua kwa msaada mashine hospitalini alikolazwa
Mwanamama akipita katika ukuta wenye picha ya Nelson Mandela mjini
Soweto. Mandela anapatiwa matibabu huko Pretoria na hali yake inaelezwa
kuwa ni mahututi na wananchi wamekuwa wakimwombea nafuu ya haraka
Mandela (94) amelazwa katika Hospitali ya Magonjwa ya Moyo, Med – Clinic, Pretoria kwa siku ya 19 sasa na taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na Ikulu ya Afrika Kusini tangu Jumapili, usiku zinathibitisha kwamba hali yake ni mahututi.
Mandela (94) amelazwa katika Hospitali ya Magonjwa ya Moyo, Med – Clinic, Pretoria kwa siku ya 19 sasa na taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na Ikulu ya Afrika Kusini tangu Jumapili, usiku zinathibitisha kwamba hali yake ni mahututi.
“Tunasubiri habari mbaya za kifo cha Mandela maana
taarifa zinazotolewa na Serikali kuhusu hali ya afya yake ni dalili
kwamba hawezi kuishi tena,” alisema mkazi wa Johannesburg, Doroth Nyathi
alipozungumza na mwandishi wetu na kuongeza:
“Watu wanaamini kwamba Mandela ameshafariki dunia,
lakini Serikali na familia yake wanatuficha tu, labda wanasubiri
maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa mwezi ujao.”
Mandela anafikisha umri wa miaka 95 Julai 18 mwaka
huu, lakini kuna wasiwasi kwamba huenda asiifikie siku hiyo ambayo ni
maarufu kama “Mandela Day” kutokana na kuzorota kwa afya yake.
“Kama mtu hajafa mnawezaje kukaa kujadili mahali
pa kumzika, ndiyo maana nimekwambia ni dhahiri kwamba Mzee Madiba
(Mandela) tayari amefariki, ila wanatuficha tu,” alisema Nyathi.
Nyathi alikuwa akirejea taarifa za vyombo vya
habari kwamba familia ya Mzee Mandela ilikutana katika kikao cha siri
juzi kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 08:00 mchana kujadili “mahali pa
maziko” ya shujaa huyo aliyeongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi,
kufungwa jela miaka 27 na baadaye kuwa Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika
Kusini.
Habari kutoka katika kikao hicho kilichohudhuriwa
na waziri katika Serikali ya Afrika Kusini ambaye pia ni mwanafamilia wa
Mandela na mmoja wa viongozi wa vyama vya siasa, zinasema baadhi
walikuwa wakitaka azikwe alikozaliwa huko Mvezo, wakati wengine wakitaka
azikwe Qunu.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Afrika Kusini
vimesema Mandela atazikwa Qunu, taarifa ambazo hata hivyo,
hazijathibitishwa na Serikali ya Afrika Kusini ambayo imekuwa
ikisisitiza kwamba “Familia ya Mandela isaidiwe katika kipindi hiki
kigumu.”
Kwa upande wake, mkazi wa Pretoria, Lisa Wright
alisema wasingependa kumpoteza Mandela lakini kwa jinsi hali
inavyoendelea ni dhahiri kwamba maradhi yanamzidi nguvu hasa kutokana na
umri mkubwa.
“Tutamkumbuka sana Mzee Mandela, amechangia kufuta
uhasama baina ya watu weupe na weusi hasa kutokana na moyo wake wa
kusamehe baada ya kutoka gerezani, hivi leo suala siasa za ubaguzi
litageuka historia hasa baada ya kizazi hiki kupita,” alisema Lisa.
Hali ilivyo nyumbani
Nyumbani kwa Mandela, eneo la Houghton, Mtaa wa Laan 12 jijini
Johannesburg, watu kwa makundi wamekuwa wakifika na kuweka maua kwenye
vitalu vinavyozunguka makazi yake na wengine wakiandakia ujumbe wa
kumtakia heri ya kupona haraka kwenye mawe madogomadogo yaliyoko kwenye
vitalu hivyo.
Makazi hayo pia yamezungukwa na magari
yanayotumiwa na waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali, ambao kwa
zaidi ya wiki tatu wameweka kambi katika eneo hilo tangu kuripotiwa
kuzorota kwa afya ya kiongozi huyo.
No comments: