Ads Top

Kutoka Chama Cha Mapinduzi CCM:Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula Ala Chakula Cha Jioni na Ujumbe Maalum Kutoka Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO)

 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayseer Khalid, kwenye chakula cha jioni, alichomwandalia mgeni huyo na ujumbe wake, kwenye hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam, Jini 12, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Mangula akifurahi hapa na apale na wageni kabla ya chakula
 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama Cha PLO,Jehad Abu Znead (kushoto) akimsalimia Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Khamis Dadi kwenye hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, wakati wa chakula cha jioni ambacho Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula aliuandalia ujumbe wa PLO uliopo nchini, Juni 12, 2013. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Amina Makilagi, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Kiongozi wa zamani wa Makao Makuu ya CCM, Hulda Kibacha.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akimsalimia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama cha PLO, Jehad Abu Znead wakati wa chakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa PLO ulipo nchini, kwenye hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC,
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza wakati wa chakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) kwenye Hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2013. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya PLO, Jehad Abu Znead  na Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Balozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujais na  Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid.
 Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer akizungumza kwenye chakula hicho.
 Mkao mzima uliokuwa hivi
 Mangula na Tayseer wakiongoza kuchukua chakula
 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Tayseer Khalid akimpa zawadi maalum, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mangula kwa ajili ya ujumbe wa PLO uliopo nchini, katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2013.
 Naam zawadi hii ni nzuri: Mangula akifurahia zawadi hiyo
Balozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujais (kulia) akitoa neno la kumshukuru Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula ( wapili kushoto), kwa achakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa PLO uliopo nchini, katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.