Mamia ya Watu Walivyojitokeza Wakati Mwili wa Msanii Albert Mangwea Ulipowasili Jana Mkoani Morogoro Jana Kwa Ajili ya Mazishi Leo
Sehemu ya pikipiki na umati wa watu waliokuwa pembezoni mwa barabara kushuhudia msafara huo.
Abiria
waliokuwa wakisafiri na Basi la Aboud, wakiwa wameteremka chini baada
ya magari yote yaliyokuwa yakielekea jiji Dar kutoka Morogoro kuzuiliwa
kwa muda ili kupisha msafara wa magari yaliyokuwa yakiongozana na msiba
wa Msanii Albert Mangwea, wakati ukiwasili mjini Morogoro jana jioni,
ambapo umati wa watu ulijitokeza kuanzia Mikese kwa ajili ya kumpokea
huku msafara huo ukidakwa na mapikipiki yapatayo kama 500 yaliyoanza
kuongoza msafara huo kuelekea nyumbani kwa wazazi wa marehemu huku
ulinzi ukiimarishwa zaidi kila kona ya mji huo wakati msafara huo
ulipowasili.
Askari wa usalama barabarani, akiongoza magari hayo wakati yakiwasili mjini Morogoro jana jioni kwa ajili ya mazishi leo
Msafara
huo ukipokelewa na Pikipiki maarufu kama Bodaboda zilizoanza kuongoza
msafara huo kwa mwendo wa pole hadi nyumbani kwa marehemu
Msanii Afande Sele, akiwapokea wageni waliowasili na msafara huo.....
Askari akitanga kiatu alichokiokota baada ya raia kusukumana eneo hilo wakigombea kuona jeneza lenye mwili wa marehemu.
Ulinzi pande hizi za nyumbani uliimarishwa kama hivi.Picha zote na Sufiani Muhidini
No comments: