Mwenyekiti wa Cuf, Profesa Ibrahimu Lipumba amesema Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2013/14, inategemea misaada kutoka nje na kwamba haionyeshi wazi upembuzi yakinifu wa miradi ya maendeleo
Pia, amesema bajeti hiyo inaonyesha kuwa deni la
Taifa linakuwa kwa kasi na kufikia asilimia 50 kitu ambacho ni hatari
kwa uchumi wa taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, wakati akichambua baadhi ya mambo yaliyomo kwenye bajeti hiyo,
Profesa Lipumba ambaye pia kitaaluma ni mchumi alisema bajeti ya mwaka
wa fedha 2013/14 imejaa kasoro lukuki.
Alisema tatizo lililosababisha kujitokeza upungufu
kwenye bajeti hiyo ni Serikali kuanza kujadili matumizi bila kujua
mapato yaliyopo ni kiasi gani.
“Bajeti yetu imejaa matatizo mengi, kwanza
haionyeshi wazi upembuzi yakinifu kwenye miradi ya maendeleo jambo
ambalo ni la ajabu,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza: “Ni jambo la
kushangaza kuona bajeti ya maendeleo ambayo ndiyo muhimu kwa uchumi wa
nchi inategemea mikopo ya nje, misaada ya nje na mikopo ya ndani jambo
ambalo linazidi kuliongeza Taifa mzigo wa madeni.”
Profesa Lipumba,alifafanua kuwa utaratibu mzuri
ambao nchi nyingi za Afrika zinatumia katika kuwasilisha bajeti za nchi
zao ni kujua kwanza mapato ya nchi ndipo wapange matumizi ya Serikali
tofauti na sisi tunavyofanya.
Profesa Lipumba alitoa mfano kuwa mara nyingi
wamekuwa wakiomba kujua upembuzi yakinifu kwenye mradi wa bomba la gesi
kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam, lakini jambo hilo limekuwa gumu na
limejaa usiri mkubwa.
Ajira
Akizungumzia suala la ajira alisema, Serikali imekuwa na kigugumizi kueleza wazi mwaka huu wa fedha imeajiri watu wangapi.
Alisema “Bajeti ya mwaka jana ilieleza wazi imetoa
ajira 7000, lakini mwaka huu wa Serikali imekuwa ikizunguka bila
kueleza wazi itatoa ajira kiasi hagi jambo ambalo ni la kushangaza
No comments: