WATU 7 WAJERUHIWA NA MLIPUKO WA 'BOMU' KWENYE MKUTANO MKUBWA WA CHADEMA WA KUHITIMISHA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA MADIWANI SOWETO ARUSHA
Picha juu ni sehemu ilyotapakaa damu muda mfupi baada ya bomu kulipuka kwenye mkutano wa kampeni wa chadema Soweto Arusha
Baadhi ya majerihi wakiwapatiwa huduma ya kwanza muda mfupi baada ya bomu kulipuka kwenye mkutano wa chadema Soweto Arusha
Baadhi ya nguo,viatu na damu vikiwa vimetapakaaa muda mfupi baada ya bomu kulipuka kwenye mkutano wa chadema Soweto
Baadhi ya wanachama wa chadema waliyojeruhiwa vibaya baada ya bomu kulipuka kwenye mkutano wa chadema soweto arusha
Baadhi
ya vijana wakiwa nje ya kituo kidogo cha polisi mbauda wakisisitiza
kuachiwa kwa 75 waliyokamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi arusha
waachiwe
Helikopta
ikitu kwenye uwanja wa Soweto Arusha leo na Mwenyekiti wa Chadema na
Mbunge wa Hai Freeman Mbowe muda mfupi kabla ya Bomu kulipuka kwenye
mkutano wa chadema
Sehemu
ya Mamia na Maelfu ya wananchama wa chadema wakiwa wamefurika viwanja
vya soweto arusha leo kwa ajili ya kufunga kampeni za udiwani kata nne
kwa ajili ya jiji hilo ambapo muda mfupi baadae kulitokea mlipuko wa
bomu.Picha Zote na Mohamedi Mtoi
Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa
kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA
katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga
kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.
Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali za Seliani na Mount Meru ambapo baadhi ya watu wamejitolea vyombo binafsi vya usafiri na wengine wanashirikiana na Madaktari na Wauguzi wa hospitali hizo kutoa huduma ya kwanza.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali hizo.
Bomu hilo linaelezwa kuwa lilipuka kwenye mkusanyiko wa watu meta chache kutoka jukwa kuu, mwendo wa saa kumi na mbili kasoro robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo hilo

No comments: