Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameambia taifa hilo lianze kujiandaa kwa sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Mandela tarehe 18 mwezi Julai
Mandela ambaye anaheshimika sana kote duniani, atafikisha umri wa
miaka 95,lakini kwa sasa angali mahututi hospitalini mjini Pretoria.
Alilazwa hospitalini tarehe 8 mwezi Juni akiwa na maradhi ya mapafu.
Kauli ya Zuma inakuja baada ya mke wa zamani wa
Mandela Winnie Mandela, kukashifu chama ha ANC kwa kumnasa kwa video
Mandela, walipomtembelea kwake nyumbani mwezi Aprili.
Kanda hiyo ilionyesha Mandela akiwa na mshangao na bila ya tabasamu wakati wa ziara ya mmoja wa vigogo wa ANC nyumbani kwake.
Winnie Madikizela-Mandela, alisema "kweli siwezi
kueleza ambavyo familia ilihisi uchungu kuhusiana na kanda hiyo, na
haikupaswa kwa jambo hilo kufanyika.''
Ikijibu tuhuma hizo, chama cha ANC kilitetea ziara hiyo, kikisema kuwa haikuwa na njama ya kutaka kujitafutia umaarufu.
Hapo Jumatatu, rais alitoa taarifa kusema kuwa wananchi wa Afrika Kusini waanze kujiandaa kwa sherehe za kuzaliwa kwa Madiba.
"lazima sote tufanye angalau jambo zuri kwa sababu ya utu kwa siku hiyo kama ujumbe wetu mzuri kwa Mandela,'' alisema Zuma.

Tanzanian Shilling Converter
No comments: