Rais wa Marekani Barack Obama ameweka mauwa kwenye makaburi ya waathiriwa wa mashambulizi ya mabomu dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 1998, kama ishara ya kuwakumbuka
Raia 11 wamarekani waliuawa katika shambulizi hilo lililofanywa na
kundi la kigaidi la al-Qaeda ambaklo lilifanyika wakati mmoja na
shambulizi lililofanywa dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Nairobi,
Kenya.
Obama aliuungana na rais mstaafu wa Marekani George W Bush kwa kumbukumbu hizo.
Rais Obama yuko katika mkondo wa mwisho wa ziara
yake ya pili ya Afrika akiwa rais , ambapo alitembelea Senegal na
Afrika Kusini.
Aidha Obama pia atamtembelea kituo cha
kuzalishha umeme kinachomilikiwa na Marekani nchini humo, kufuatia
tangazo lake mwishoni mwa wiki la mradi wa umeme utakaogharimu mabilioni
ya dola.
Mradi huo wa miaka mitano, unatarajiwa kusaidia
kuongeza kasi ya uzalishaji wa umeme kusini mwa jangwa la Sahara,kwa
ushirikiano na mataifa ya kiafrika pamoja na sekta binafsi.
Akiwa nchini humo, Obama pia anatarajiwa
kuzindua mpango unaonuia kusaidia nchi za Afrika Mashariki ikiwemo,
Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda kushirikiana kibiashara.
Wakati huohuo, mkewe Obama, Michelle anatarajiwa
kuhudhuria mkutano wa wake za marais, unaoandaliwa na taasisi ya George
W Bush huku ukiongozwa na mkewe Laura Bush.

Tanzanian Shilling Converter
No comments: