KESI ya kudaiwa kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao Meneja wa Hoteli, Goodluck Kuyumbu inayomkabili Staa wa Filamu, Wema Isaac Sepetu imeunguruma Jumatano iliyopita katika Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar na watu kufurika pomoni, Ijumaa linakumegea kilichojiri
KESI
ya kudaiwa kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao Meneja wa
Hoteli, Goodluck Kuyumbu inayomkabili Staa wa Filamu, Wema Isaac Sepetu
imeunguruma Jumatano iliyopita katika Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar
na watu kufurika pomoni, Ijumaa linakumegea kilichojiri
Katika
mahakama hiyo watu walifurika kwa lengo la kutaka kumuona Wema
aliyepandishwa mbele ya Hakimu, Bernice Ikanda kusomewa mashtaka ya
kudaiwa kufanya vurugu, kushambulia kwa kumpiga makofi na kumtukana
Goodluck.
ATINGA NA MSAFARA
Wakati wa kuwasili mahakanai hapo, Wema aliambatana na msafara wa magari matatu, yeye akiwa katika lake la aina ya Audi Q 7, magari mengine yalikuwa ni Toyota Opa na Toyota Hiace yaliyokuwa na watu wake.

WATU WAFURIKA MAHAKAMANI
Kutokana na jamii kupenda kufuatilia matukio ya kila siku ya Wema, watu kibao walifika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo.
Mara baada ya mlimbwende huyo wa mwaka 2006-07 kuzama katika chumba cha mahakama, kulitokea vurugu kwa baadhi ya watu kukanyagana ili kutaka kumuona na kusikilza kesi hiyo kwa ukaribu zaidi.

AINGIZWA CHUMBA CHA MAHAKAMA
Wema aliingizwa katika chumba cha mahakama sambamba na Goodluck ambapo Hakimu Bernice alianza kumuuliza mlalamikaji kama alikuwa na mashahidi walioshuhudia tukio hilo lilivyotokea.
Goodluck alijibu kuwa anao mashahidi na kumwambia hakimu kwamba anaweza kuwaleta mbele ya mahakama hiyo.

KESI YAPIGWA KALENDA TENA
Hakimu aliamuru kesi hiyo iahirishwe hadi Agosti 20, mwaka huu na kumtaka mlalamikaji kufika na mashahidi wake.
Kuonesha kwamba watu wengi walikuwa wamefika kushuhudia kesi hiyo, walitawanyika baada ya uamuzi huo

No comments: