Mahakama katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville imeanza kusikiliza kesi dhidi ya wanajeshi 23 walioshtakiwa kwa kosa la kusababisha mlipuko katika ghala la silaha mjini humo
Zaidi ya watu miambili walifariki na wengine elfu mbili miatatu kujeruhiwa kwenye milipuko hiyo mwezi Machi mwaka jana.
Milipuko ilisikika umbali wa
kilomita nyingi katika nchi jirani ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo
na kuharibu madirisha na paa za nyumba mjini Kinshasa. Wanajeshi hao
wameshtakiwa kwa kosa la kuanzisha moto ulioteketeza bohari hilo kwa
maksudi.
Majaji kadhaa waliapishwa siku ya Ijumaa ili
kusikiliza kesi hiyo ambayo wanajeshi 20 wanashitakiwa pia kwa kosa la
kutishia usalama wa nchi.
Milipuko hiyo iliharibu nyumba nyingi na kuwaacha zaidi ya watu 17,000 bila makao.
Uchunguzi katika kesi hiyo ulisababisha
kukamatwa kwa watu 26 akiwemo naibu mkuu wa baraza la usalama wa kitaifa
ingawa raia watatu waliokuwa wamekamatwa waliachiliwa.
Kwa mujibu wa taarifa za gazeti pekee
linalochapishwa kila siku, Les Depeches de Brazzaville, lilinukuu
taarifa iliyosema kuwa vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo
vitapeperushwa moja kwa moja katika baadhi ya vituo vya redio na
televisheni.
No comments: