SHEREHE ZA MAGEREZA ZA KUPONGEZANA USHINDI WA JUMLA MAONESHO YA NANE NANE ZAFANA DODOMA
Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Nassoro Patrick akikabidhi Kombe la
Ushindi wa kwanza wa jumla wa Maonesho ya Wakulima kwa Mgeni rasmi
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro aliyemwakilisha
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini katika hafla fupi ya kuwapongeza
Maafisa na Askari walioshiriki Maonesho ya Wakulima Kitaifa
yaliyofanyika Uwanja wa Nzuguni, Dodoma. Sherehe hizo zimefanyika jana
katika Ukumbi uliopo katika Ofisi ya Magereza Mkoa, Dodoma
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro akitoa hotuba
kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini wakati wa hafla fupi
ya kuwapongeza Maafisa na Askari washiriki wa Maonesho ya Wakulima
Kitaifa kwa kufanikisha ushindi wa kwanza wa jumla. Sherehe hizo
zimefanyika jana katika Ukumbi uliopo Ofisi ya Magereza Mkoa
Dodoma
Makamanda wa Jeshi la Magereza wakisakata rumba wakati wa hafla fupi ya
kupongezana baada ya kutwaa Ushindi wa kwanza wa jumla katika Maonesho
ya Wakulima Kitaifa yaliyofanyikia Uwanja wa Nzuguni, Dodoma. Sherehe
hizo za kupongezana zimefanyikia katika Ukumbi wa Ofisi ya Magereza
Mkoani Dodoma
Baadhi ya Maafisa na Askari washiriki wa Maonesho ya Wakulima Kitaifa
wakiwa katika hafla fupi ya kupongezana baada ya kutwaa ushindi wa
kwanza wa jumla wa Maonesho ya Wakulima Kitaifa yaliyofanyika Uwanja wa
Nzuguni, Dodoma.Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
Jeshi la Magereza Nchini limeibuka tena Mshindi wa kwanza upande wa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwenye Maonesho ya Wakulima maarufu Nane
Nane yaliyofanyika Uwanja wa John Mwakange, Jijini Mbeya katika Kanda ya
Nyanda za juu Kusini ikishirikisha Mikoa ya Rukwa, Ruvuma, Iringa na
Mbeya ambapo Mgeni rasmi katika Kilele cha Maonesho hayo alikuwa ni
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Capt. Mstaafu Aseri Msangi.
Jeshi la Magereza Tanzania Bara ni miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyochini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo Jeshi la Magereza limeshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo ya Wakulima ambayo leo hii yanafikia Kilele katika Kanda mbalimbali na Kitaifa yalifanyika jana Agosti 07, 2013 katika Uwanja wa Nzuguni, Dodoma na Mgeni rasmi katika Kilele cha Maonesho hayo alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Iddi
Mbali na ushindi huo katika Kanda ya Nyanda za juu Kusini pia Jeshi la Magereza Nchini limeshiriki Maonesho hayo katika Kanda ya Kasikazini ikijumuisha Mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha ambapo Jeshi la Magereza limefanikiwa kushika nafasi ya pili kwa upande wa Taasisi za Uzalishaji za Serikali na Maonesho hayo yamefungwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu.

Ushindi huo ni wa mfululizo kwani jana Agosti 07, 2013 Jeshi la Magereza Nchini liliibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika Kilele cha Maonesho ya Wakulima maarufu Nane Nane Kitaifa yaliyofanyika katika Uwanja wa Nzuguni, Dodoma na ushindi mwingine katika Kanda ya Magharibi-Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora na Kanda ya Mashariki iliyojumuisha Mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Morogoro ambapo kufuatia ushindi huo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja alipokea ushindi huo kwa furaha kubwa na kutoa Salaam za pongezi kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza walioshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo.
Imetolewa na Mkaguzi wa Magereza, Lucas Mboje,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza nchini,
Agosti 08, 2013.
No comments: