Watendaji Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Wapewa Mafunzo ya Bajeti Kijinsia
Meza kuu ikiwasilisha hotuba zake kwa washiriki wa mafunzo.
Mkurugenzi wa Mashirika yasio ya Kiserikali toka wizara hiyo, Marcel Katemba akisoma hotuba ya Katibu Mkuu
Mkurugenzi wa Mashirika yasio ya Kiserikali toka wizara hiyo, Marcel Katemba akizungumza kabla ya kufungua mafunzo.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo hayo ya kijinsia
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada anuai.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada anuai.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
Watendaji Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Wapewa Mafunzo ya Bajeti Kijinsia .
Na Mwandishi wa Thehabari.com
VIONGOZI
wakuu na watendaji wa idara mbalimbali kutoka Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto nchini leo wamepewa mafunzo ya namna ya kuandaa
bajeti kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Mafunzo
hayo ya siku nne yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) yameandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kupitia taasisi
yao ya Chuo cha Jinsia (GTI), ambapo washiriki hao kutoka Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wanawezeshwa kuandaa bajeti kwa
mtanzamo wa kijinsia.
Akizungumza
katika mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya alisema
mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yanasaidia kujenga stadi na maarifa kwa
viongozi na watendaji wakuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto kuzingatia masuala ya jinsia kwenye bajeti ya Wizara hiyo.
Alisema
ni mafunzo yanayounganisha utashi wa kisiasa kwa kuzingatia masuala ya
jinsia na usawa serikalini, ili kupunguza mapengo yaliyopo inabidi
kuwekeza fedha na rasilimali anuai.
alisema
nadharia iliyopo kwenye sera inaweza kutekelezeka endapo kutakuwa na
uwezeshaji wa rasilimali na fedha ili kuhakikisha huduma za kijamii
zinatekelezwa kwa kuzingatia mahitaji ya makundi yote yaani wanawake na
wanaume.
No comments: