Ads Top

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAM KINANA NDANI YA BUTIAMA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu  Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kyabakari kata ya Kyokilango ambapo aliwaeleza wananchi wa Butiama kama ni watu wenye heshima sana nchi hivyo aliwasihi watu kufuata yale aliotuachia Baba likiwemo suala la Ujamaa ,kujitegemea na uadilifu miongoni wa viongozi.
 
Bibi Safina Kombo balozi mstaafu akielezea matatizo yanayowapata wajane kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea shina namba 12 tawi la Butiama.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Kyabakari kata ya Kyokilango  wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Mbunge wa Butiama Vijijini, Ndugu Nimrod Mkono akizungumza na wakazi wa shina namba 12 tawi la Butiama ambapo aliahidi kuwasogezea kisima cha maji kiwe karaibu zaidi na wakazi hao.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa akisalimiana na mdogo wa Mwalimu Nyerere, Daniel Nyerere walipokutana kwenye kikao cha Balozi wa shina namba 12 tawi la Butiama.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na mdogo wa Mwalimu Nyerere ,Daniel Nyerere walipokutana kwenye kikao cha Balozi wa shina namba 12 tawi la Butiama.
“Nape endelea kupambana” ndivyo anavyoonekana akiambiwa na mdogo wa Mwalimu, Daniel Nyerere.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya kata ya Busegwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwa ameshikilia maru maru (tiles) pamoja na Mbunge wa jimbo la Butiama vijijini Ndugu Nimrod Mkono ambapo mbunge huyo amejitolea bati zaidi ya mia tatu pamoja na tiles na milango yote.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.