KUTOKA JESHI LA MAGEREZA: KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, JOHN CASMIR MINJA AHUDHURIA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA
Askari wa Magereza wa Zambia wakipita mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri
wa Mambo ya Ndani wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu(hayupo pichani) katika
Mwendo wa haraka kama wanavyoonekana Kikakamavu wakati wa Maadhimisho ya
Magereza Day ya Zambia ambapo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini
Tanzania, John Casmir Minja hivi karibuni alihudhuria Maadhimisho ya
Siku ya Magereza huko Kabwe, Zambia.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir
Minja(wa tatu kulia) akiwa amesimama katika Jukwaa Kuu kupokea heshima
wakati Gwaride la Askari wa Magereza wa Zambia likipita mbele ya Mgeni
Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza nchini Zambia Septemba 26,
2013 (wa kwanza kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia(Mb) Mhe.
Edgar Lungu. Wengine ni Mkurugenzi wa Magereza anayesimamia Uzalishaji
na Urekebishaji katika Taifa la Sudani Kusini(wa kwanza kulia) akiwa na
Mkurugenzi Msaidizi wa Magereza.
Mkuu wa Jeshi la Magereza Zambia, Kamishna wa Magereza Percy
Chato(wa kwanza mstari wa kwanza) akiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza
Tanzania, John Casmir Minja(wa kwanza mstari wa pili) wakiangalia Gwaride
Maalum la Maadhimisho ya Siku ya Magereza nchini Zambia. Maadhimisho
hayo yamefanyika hivi karibuni Septemba 26, 2013 katika Chuo cha Mafunzo
ya Maafisa Magereza, Kabwe Zambia.
Mkuu wa Jeshi la Magereza Zambia, Kamishna wa Magereza Percy Kato(
wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa
Magereza Tanzania, John Casmir Minja(wa tatu kulia) alipotembelea Ofisi
za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Zambia kufuatia Mwaliko rasmi wa
Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Magereza Zambia
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia,
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na
Usalama wa Zambia pamoja na Viongozi Waandamizi wa Serikali(wa tatu
kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
No comments: