Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa Aendelea na Ziara Yake Ya Kikazi Nchini Marekani Ya Kutafuta Ufumbuzi Wa Tatizo La Kiuchumi,Makampuni Makubwa Nchini Marekani Yaahidi Maelfu ya Ajira

Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akipokelewa na viongozi wa Chuo Kikuu cha Central piedmont

Mitambo
maalum inayotumika katika mafundisho ya viwandani. Hii ni kwa ajili ya
kuwafundisha wanafunzi wanaochukua kozi ya kuendesha mashine viwandani.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akitizama kwa umakin jinsi mitambo hii ya kisasa inavyofanya kazi kati hiki chuo

Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akionyeshwa jinsi mitambo ya kisasa inayotumika katika mafunzo
inavyofanya kazi. Hii karakana ndiyo inayotumika kuwatayarisha vijana
kuwa wabunifu na kuweza kijiajiri

Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akiwa kwenye maongezi na Rais wa Chuo cha Piedmont


Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa pamoja na viongzi wa juu wa Charlotte Chamber of commerce kwenye
picha ya pamoja baada ya kufanya maongezi ya ushirikiano wa kibiashara.Picha Zote na Chadema
Leo
asubuhi Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mh. Wilbrod
Slaa Washington DC kuelekea jimbo la North Carolina ambako amelakiwa na
Rais wa Chuo cha Piedmond Community College yenye jumla ya campuses 16.
Na jumla ya wanafunzi 85,000
Piedmont
Community College ndio moja ya Community colleges bora zaidi Marekani,
na imekuwa ikitayarisha wanafunzi mahiri kwenye eneo la engineering.
Lengo
kubwa la kiongozi huyu maarufu nchini kukutana na Rais wa Chuo, ni
kujifunza siri ya mafanikio ya chuo hicho, kwa ajili ya kuwawezesha
wanafunzi wa kitanzania kufanya vizuri zaidi kwa lengo kubwa la
kutayarisha rasilimali watu. Dr. Slaa pamoja na chama cha Chadema,
wanaamini kwamba, ili kuliokoa taifa, lazima elimu ipewe nafasi ya
kwanza
Kadhalika,
Dr. Slaa na Rais was chuo kikuu cha Pedmont walikubaliana kuanzisha
program maalum itakayowawezesha vijana wa kitanzania na wakimarekani
kuanzisha urafiki utakaoziwezesha chuo hicho maarufu kufanya kazi kwa
ukaribu na vyuo vya kitanzania. Vyuo vya kitanzania vitanufaika zaidi
hasa kutokana na technologia ya kipekee ambayo hipo chuoni hapo.
Baada
ya miaka 52 ya ufisadi na kuuzwa kwa rasilimali za nchi, elimu duni,
umasikini wa kupindukia, huku taifa likiendelea kuwa omba omba Dr. Slaa
pamoja na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo imeamua kutafuta njia
mbadala ya kuleta ukombozi karibu na wananchi. Chadema imeanza kutafuta
mbinu za kumkomboa mtanzania kutoka kwenye ufukara. Lengo la Chadema ni
kutengeneza mamilioni ya ajira ambazo makampuni mengi yako tayari
kuyazalisha kama Chadema itatengeneza mazingira mazuri ya wao kuwekeza.
Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa amemaliza ziara ya siku moja carolina na kuondoka kuelekea Atlanta
georgia ambako atakutana na viongozi wa shirika la Coca-Cola, AT & T
pamoja UPS
No comments: