TAARIFA MUHIMU KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHINI:KIMBUNGA CHA “OPERESHENI KIMBUNGA” AWAMU YA PILI CHAWAKUMBA WATUHUMIWA WA UJAMBAZI, WAHAMIAJI HARAMU NA KUFUKUA SILAHA, RISASI NA VIELELEZO VINGINE – NI MPAKA KIELEWEKE
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Operesheni Kimbunga
awamu ya Pili iliyoanza tarehe 21 Septemba, hadi kufikia tarehe
01 Oktoba, 2013 imekamata watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha 88.
Kati ya hawa, 27 walikamatwa mkoani Kigoma, 43 mkoani Geita na 18 mkoani
Kagera. Watuhumiwa hawa wanaendelea kushikiliwa kwa uchunguzi
zaidi ili hatimaye wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Wakati huo huo,
Operesheni hii imefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wa uhamiaji haramu
425, kati yao 166 walikamatwa mkoani Kigoma, 50 mkoani Geita na 209
mkoani Kagera.
Wengine waliokamatwa
ni watuhumiwa wa ujangili 11, kati yao sita mkoani Kigoma na watano
mkoani Geita, na watuhumiwa watano kwa kuhifadhi au kutorosha wahamiaji
haramu kati yao wane kutoka mkoa wa Kigoma na mmoja, mkoa wa Geita.
Vitu vingine vilivyokamatwa
katika Operesheni hii ni SMG 3, Pistol 2 mkoani Kigoma na Gobole 18,
moja mkoani Kigoma na 17 mkoani Geita. Vingine ni risasi 471 za (SMG/SAR),
Star Pistol 13, Magazine za SMG 2, Sare 1 ya Jeshi la Burundi na Shati
moja, vyote katika mkoa wa Kigoma.
Vingine ni bomu
moja la kurushwa kwa mkono mkoani Kigoma, ngombe 2220 katika Hifadhi
ya Taifa ya Biharamulo mkoani Kagera, gunia 100 za mkaa mkoani Geita,
gongo lita 271, mkoani Kigoma 11 na 260 mkoani Geita. Nyara za
Serikali zilizokamatwa ni ngozi ya mbweha moja na meno matatu ya Kiboko
mkoani Geita. Bangi kilo tatu na nyavu haramu za uvuvi (makokoro)
12 pia zilikamatwa mkoani Geita.
Akizungumza katika
Mkutano na Waandishi wa habari mjini Bukoba leo, Naibu Kamishna wa Polisi
(DCP), Simon Sirro, kwa niaba ya Operesheni Kamanda wa Operesheni Kimbunga,
alisema haieleweki ni vipi watendaji wa Vijiji, Kata na Tarafa wanashindwa
kutoa taarifa kuhusu wahalifu katika maeneo yao, wakiwepo wahamiaji
haramu, na kuwa viongozi hawa wanawajibika na uhalifu unaotokea katika
maeneo yao.
Alisema ni imani
ya watendaji wa Operesheni Kimbunga kuwa Watendaji hawa wataanza kuwajibika
ili kukomesha matukio ya uhalifu hapa nchini.
IMEANDALIWA NA TIMU YA HABARI – OPERESHENI
KIMBUNGA
No comments: