Polisi katika eneo la Mtwara Kusini mwa Tanzania wamewazuilia watu wanaoshukiwa kuhudhuria mafunzo ya kundi la kigaidi la Al - Shaabab

Polisi walisema walipokea taarifa wiki moja kabla ya kukamatwa kwa washukiwa
Washukiwa walikamatwa Jumatatu katika eneo la milimani baada ya
wananchi waliowaona msituni wakifanya mazoezi ya kijeshi kutoa habari
kwa polisi
Kwa mujibu wa kamanda mkuu wa jeshi
eneo la Mtwara,Zelothe Stephens, washukiwa hao 11 walikamatwa katika
eneo la milimani la Makolionga wakiwa na nyaraka na kanda za video zenye
mafunzo ya kundi la Al Shaabab.
Washukiwa pia walikuwa na silaha zilizokuwa zimetengezwa kienyeji tu.
Zaidi ya hayo, kamanda huyo wa polisi alisema
walipokea taarifa za wananachi wiki moja iliyopita, kuhusu kundi hilo
ambalo lilikuwa linapata mafunzo msituni.
Polisi wangali wanawahoji washukiwa hao wakitaka kujua miongoni mwa mambo mengine wadhamini na wafadhili wao.
Kamanda wa polisi alimtaja kiongozi wa kundi hilo kuwa Mohammed Makande mwenye umri wa miaka 39.
Kwa mujibu wa polisi, washukiwa watafikishwa mahakamani mara baada tu ya uchunguzi kukamilika.
Kumakatwa kwao kunakuja wakati ambapo visa vya
ugaidi vimeongezeka katika kanda ya Afrika Mashariki hususan nchini
Kenya na Somalia.
Wiki jana Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete,
aliwataka wananchi kuchukua hatua zaidi huku serikali ikidhibiti hali ya
usalama katika maeneo yaliyo katika hatari ya kushambuliwa.
No comments: