Rais JK aanza ziara ya siku tano ya mkoa wa pwani, afungua Gati la Mafia

Gati ya Mafia iliyofunguliwa rasmi na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mjini Mafia leo

Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Gati la Mafia
iliyojengwa wilayani Mafia leo.Kushoto ni Waziri wa Uchukuzi
Dkt.Harrison Mwakyembe. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Mafia Mheshimiwa
Abdul Karim Shah,Wantatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi.Mwantum
Mahiza na kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete

Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitembea juu ya Gati la Mafia lenye urefu wa
kilometa moja na nusu muda mfupi baada ya kulifungua rasmi mjini Mafia
leo.Wengine katika picha kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi.Mwantumu
Mahiza, wa pili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,wa nne kushoto
ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia Bi. Sauda Mtondoo na kulia ni mbunge wa
Mafia Mhe.Abdul Karim Shah.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
Imetolewa na:
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka
Watanzania kuachana na hulka ya kukejeli jitihada za maendeleo na kujenga
fitina kuhusu miradi ya maendeleo.
Amesema
kuwa baadhi ya Watanzania, badala ya kuunga mkono jitihada za maendeleo,
wanapiga kasi mpya ya kurudi nyuma kwa kupinga na kukejeli miradi ya maendeleo.
Rais
Kikwete alikuwa anazungumza leo, Alhamisi, Oktoba 3, 2013, Kisiwani Mafia
wakati alipoanza ziara ya siku tano kukagua shughuli za maendeleo na kufungua
miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Pwani.
Akizungumza
na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Chuo cha Ufundi,
Tereni, nje ya mji mkuu wa Mafia wa Kilindoni, Rais Kikwete ameimwagia sifa
Mfuko wa Maendeleo ya Mafia (MIDEF)
ambao umefanikisha mambo makubwa ya maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa Chuo hicho ambacho kitagharimu kiasi cha sh. bilioni 5.33
na kuchukua wanafunzi 400 kitakapokamilika. Chuo hicho pia kitakuwa na sehemu
ya Chuo cha Michezo – Sports Academy.
Mbali
na ujenzi wa chuo hicho, MIDEF
imejenga shule ya sekondari ya bweni, imeunga mkono shule za sekondari za kata
za Serikali kwa kuzipa kompyuta na madawati, inatoa mikopo ya maendeleo kwa
wananchi, imetoa zana za kazi kwa taasisi za Serikali na imesimamia kupatikana
kwa fedha za kusambaza umeme katika vijiji vyote vya Mafia kupitia Mamlaka ya
Kusambaza Umeme Vijijini (REA).
Kwenye
mradi wa kusambaza umeme vijijini, kwa mfano, MIDEF imechangia kiasi cha Sh. Milioni 500 katika mradi ambao
utagharimu Sh. Bilioni tano.
Rais
Kikwete amewaambia wananchi wa Mafia: “Jitihada hizi za MIDEF lazima ziungwe
mkono. Sina maneno mazuri ya kuwaambieni kuwa kama hamtaunga mkono jitihada
hizo mtakuwa na matatizo, tena matatizo makubwa sana. Mtakuwa mnafikia kwa kasi
mpya ya kurudi nyuma.”
Amesisitiza
Rais Kikwete: “Nasema hivyo kwa sababu sisi Watanzania kazi yetu imekuwa ni kujenga
fitina, kubeza na kukejeli jitihada za maendeleo. Hiyo ndiyo hulka yetu kujenga
fitina kuhusu miradi ya maendeleo.”
“Tunashangaza
sana. Mtu anayekuhubiria upate maendeleo unamwona mtu mbaya, lakini mtu
anayekuhubiria usipate maendeleo unamuona mtu mzuri na mwema. Tabia hii ndiyo
naiita ya kupiga kasi mpya ya kurudi nyuma,” amesema Rais
Kikwete.
Katika
ujenzi wa Chuo hicho cha Ufundi, Serikali imechangia kwa kutoa ardhi ya kujenga
chuo hicho katika eneo la Tereni na kukamilika kwa Chuo hicho kuitaiwezesha
Tanzania kuongeza idadi ya vyuo vya ufundi nchini. Kwa sasa kuna vyuo vya
ufundi 742 vyenye wanafunzi 145,510, kati ya hivyo 17 vikiwa vya Serikali, na
vilivyobakia vikiwa vya watu na taasisi binafsi.
Rais
Kikwete ambaye ameshinda siku nzima katika Wilaya hiyo ya Mafia amerejea Dar Es
Salaam jioni ya leo na kesho atafanya ziara ya Wilaya ya Mkuranga.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
3 Oktoba, 2013
No comments: