TAARIFA KWA UMMA KUTOKA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA:UTENDAJI KAZI WA BOYA LA MAFUTA LA SINGLE POINT MOORING (SPM) KIGAMBONI, DAR ES SALAAM

Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mafuta kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Capt. Abdul
Mwingamno akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu ufanisi wa
mradi wa SPM Ikiwa ni pamoja na kuhudumia meli kubwa zenye uwezo wa kubeba
mzigo wa tani 150,000,Wakati wa Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mafuta kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Capt. Abdul
Mwingamno akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu ufanisi wa
mradi wa SPM Ikiwa ni pamoja na kuhudumia meli kubwa zenye uwezo wa kubeba
mzigo wa tani 150,000,Wakati wa Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Mvungi
MAMLAKA
YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA
UTENDAJI
KAZI WA BOYA LA MAFUTA LA SINGLE POINT MOORING (SPM) KIGAMBONI, DAR ES SALAAM
UTANGULIZI
Mradi
wa ujenzi wa boya jipya lijukanalo kama Single Point Mooring (SPM) pamoja na
miundombinu ya kusafirisha mafuta ulianza mwaka 2010 na kukamilika mwezi
Novemba 2012.
GHARAMA YA MRADI
Mradi
huu uligharimu kiasi cha dola za Marekani millioni 70.5 sawa na Shilingi
bilioni 113 za Tanzania.
UWEZO WA BOYA
SPM
ina uwezo wa kuhudumia meli zenye ujazo wa tani 150,000 za mafutana tangu boya
hilo limezinduliwaNovemba 2012 mpaka Agosti 2013 limehudumia mafuta safi (white
products) jumla ya tani 1,529,411 na tani 513,787 za mafuta ghafi wakati mafuta
yaliyohudumiwa na Kitengo cha Mafuta cha Kurasini (KOJ) katika kipindi cha
Novemba 2012 mpaka Agosti 2013 ni tani 1,503,298.
Kukamilika
kwa mradi huu, kunaiwezesha Bandari kuhudumia meli kubwa zenye uwezo wa kubeba
mzigo wa tani 150,000 (DWT) hivyo kuongeza tija katika kuhudumia meli za
mafuta. Tofauti na boya la awali SPM sasa inaweza kupokea na kusukuma mafuta
safi (white products) na ghafi (crude oil) kwa wakati mmoja.
Mradi
wa SPM unaiwezesha nchi kupakua mafuta kwa kutumia meli kubwa zenye uzito wa
150,000 (DWT) ukilinganisha na zile zinazoleta mafuta katika gati la mafuta la
Kurasini (KOJ) zenye uzito wa 45,000 (DWT).
MAFANIKIO/UFANISI
Tangu
SPM mpya ianze kufanya kazi mnamo tarehe 15 Novemba 2012, yamepatikana
mafanikio makubwa hasa katika kupunguza msongamano wa meli za mafuta uliokuwepo
miaka iliyopita. Msongamano huo ulikuwa ni kero kubwa kwa wadau wa bandari na waagizaji
mafuta nchini.
Msongamano
huo uliibebesha Serikali mzigo mkubwa wa kulipa gharama ijulikanayo kama
‘demurrages’ ambayo wenye meli hutozabaada ya meli kusubiri muda mrefu kufunga
kwenye gati la KOJ.
Gharama
hiyo ilifikia hadi Dola za Kimarekani 50 kwa kila tani moja. Lakini kutokana na
maboresho yaliyofanyika yameweza kupunguza gharama za demurrages hadi Dola za Kimarekani 1.2 kwa kila tani. Hayo ni
mafanikio makubwa ambayo yamekuja baada ya kupunguza siku za meli kusubiri zamu
toka wastani wa siku 45 hadi siku 1.
Kwa
kuwa kituo cha Mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jetty – KOJ) kinaendelea kutoa
huduma sambamba na SPM mpya, uwezo wa kuhudumia meli umeongezeka kwa kuwezesha
kuhudumia meli mbili hadi tatu kwa wakati mmoja. Hiyo ikiwa na maana kuwa kila
kituo kinaweza kupakuwa aina tofauti ya mafuta na hivyo kuongezea ufanisi na
tija.
Mafanikio
zaidi yanategemewa muda si mrefu kwa kupunguza siku za kupakuwa mafuta SPM mara
makampuni ya mafuta yatakapomaliza uboreshaji wa mabomba yao hadi kufikia
kipenyo cha nchi 12, ikiwemo makampuni ya mafuta ya Kigamboni kuweka bomba
maalum la kupokelea mafuta moja kwa moja kutoka SPM badala ya kupitia KOJ
ambako kutokana na umbali unasababisha kasi ya ujazo kwa saa kupungua.
UTENDAJI KAZI WA BOYA
Meli
zinafungwa kwenye boya ambalo liko kwenye kina cha maji cha mita 25.5 (CD)
ambapo bomba la 24” linaleta mafuta ya Dieseli mpaka Kigamboni ambapo
linaunganika na bomba la 18” kuleta mafuta mpaka KOJ na kusambazwa kwa wenye
matanki ya kuhifadhia mafuta.
Mafuta
ghafi (crude oil) yanatolewa kwenye meli na kupitisha kwenye bomba la 28” urefu
wa bomba ni kilometa 3.7 majini na kilometa 4.3 nchi kavu mpaka Kigamboni na
kilometa 2 kutoka Kigamboni mpaka KOJ.
Mafuta
ya Petroli, mafuta ya taa (Kerosine), Mafuta ya ndege (Jet A1) na baadhi ya
mafuta ya Dieseli bado yanapitishwa KOJ.
Mipango
ya TPA, ni kukarabati boya la zamani ili mafuta ya Petroli nayo yapitie SPM.
Mabomba
ya kuleta mafuta ya Petroli (dock lines) yameongezwa na manifold mpya za
Dieseli na Petroli kujengwa SPM. Mabomba ya kuleta mafuta ya chakula nayo
yameongezwa KOJ.
Ili
kuongeza kasi ya kupakua mafuta kutoka SPM, TPA inajenga manifold mpya huko
Kigamboni kwa ajili ya OMCs waliopo Kigamboni.
MABORESHO ZAIDI
Awamu
ya pili ya mradi wa SPM itatekelezwa kati ya mwaka 2014 na mwaka 2016 na
itahusisha ujenzi wa matenki ya kupokea mafuta kwa muda (custody transfer
tanks) na kugharimu dola za Marekani milioni 60 sawa na shilingi billion 96 za
Tanzania.
MCHANGO
WA SPM KATIKA UPATIKANAJI WA MAFUTA NCHINI
Boya
la zamani la SPM lilikuwa linahudumia mafuta ghafi (crude oil) tu kwa ajili ya
Zambia na hapa nchini. Lakini mradi wa SPM umewezesha
Boya jipya la SPM kuhudumia mafuta ghafi na mafuta safi (white products).
Endapo mradi wa boya jipya usingefanyika tungekuwa tumehudumia
jumla yatani 2,017,085 tu za mafuta yaliyosafishwa na
yasiyosafishwa sawa na asilimia56.9, lakini kutokana na boya jipya
la
SPM kuhudumia tani 1,529,411 za mafuta sawa na asilimia 43.1
tumeweza kuhudumia jumla ya tani 3,546,446 katika kipindi cha
kuanzia Novemba 2012 mpaka Agosti 2013.
MWISHO
Tunawasihi wananchi wote tushirikiane katika kulilinda na
kulitunza
boya hili ambalo limeigharimu Serikali na Mamlaka fedha nyingi ili
liwezkuleta manufaa kwa uchumi wetu na wananchi kwa ujumla.
Imetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania
S.L.P. 9184
DAR ES SALAAM
No comments: