KUTOKA JESHI LA MAGEREZA NCHINI: ONA JINSI MABALOZI WA JUMUIYA YA NCHI ZA ULAYA (EU) WALIPOTEMBELEA GEREZA KUU UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM
Msafara wa Magari ya Ujumbe wa Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya
ukiwasili katika Viwanja vya Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam leo
Oktoba 10, 2013
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akisalimiana na
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Gilberto Sebregondi
ambaye aliongoza ujumbe wa Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya katika
ziara yao leo Oktoba 10, 2013 Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam
ili kujionea namna ambavyo Jeshi la Magereza linazingatia kikamilifu
masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Uendeshaji wa
Magereza hapa nchini.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( wa tatu kushoto
mstari wa pili) akiongozana na Mabalozi mbalimbali wa Jumuiya ya Nchi
za Ulaya kuelekea sehemu ya Zahanati ya ndani inayohudumia Wafungwa wa
Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam waliopotembelea leo Oktoba 10,
2013.

Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya wakiongea na Mahabusu wanaokabiliwa
na kesi za Uharamia ambapo wameiomba Jumuiya hiyo pamoja na Serikali
kuwatafutia Wakalimani ili kuwezesha kesi zao kusikilizwa kwa wakati( wa
kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir
Minja.

Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya wakiwasilikiza kwa makini Wafungwa
wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam waliohukumiwa Adhabu ya
Kunyongwa(hawapo pichani) ambapo wameiomba Jumuiya ya Ulaya kuendelea
kupaza sauti na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ili Adhabu hiyo hapa Nchini Tanzania iweze kuondelewa(wa pili kulia) ni
Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Mhe. Dianna Melrose.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) akisoma
hotuba yake fupi mbele ya Balozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya Nchini
Tanzania, Mhe. Filiberto Sebregondi(aliyeketi mbele) pamoja na Mabalozi
wa Jumuiya ya nchi za Ulaya wanaoonekana katika picha kabla ya
kutembelea sehemu mbalimbali za Gereza Kuu Ukonga leo Jijini Dar es
Salaam.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya
mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za Gereza Kuu Ukonga leo
Jijini Dar es Salaam(wa tatu kushoto) ni Balozi wa Jumuiya ya Ulaya
Nchini Tanzania, Mhe. Filiberto Sebregondi ambaye aliongoza Ujumbe wa
Mabalozi hao.
No comments: