Watu 3 akiwemo polisi wameuawa na wengine kadha kujeruhiwa kwenye ghasia katika mji wa Mombasa, Kenya, baada ya polisi kuvamia msikiti unaosemekana kutoa mafunzi ya itikadi kali za dini ya kiisilamu

Polisi walitumia moshi wa kutoa machozi na risasi za raba dhidi ya waandamanaji na kuwakamata watu 100.
Viongozi wa mombasa wamelaani kitendo cha polisi wakisema kuwa ni kinyume na sheria.
Mashekhe wawili ambao wakihubiri katika msikiti
wa Masjid Mussa walipigwa risasi na kuuliwa na watu wasiojulikana katika
miezi ya karibuni.
Polisi wa Kenya wameuhusisha msikiti huo na
kuajiri wapiganaji wa kundi la wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al
Shabaab, ambalo mwaka jana lilishambulia jumba la maduka la Westgate
mjini Nairobi.
Habari na BBCswahili.com
Habari na BBCswahili.com
No comments: