Ads Top

Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar:Mahmuod Thabit Kombo-CCM Atangazwa Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar

  Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmuod Thabit Kombo, akizungumza na Waandishi wa habari na kutowa shukrani kwa wapinga kura wake na WanaCCM waliomuunga mkono katika safari ya Kampeni na kuahidi kutimiza ahadi zote alizoahidi kwa Wananchi wa Jimbola Kiembesamaki na kuondo kero zote na kuwaletea maendeleo katika jimbo lao.
  Mgombea wa Chama cha ADC Mhe. Amani Ismail Rashid akisaini fomu ya Matekeo ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbola Kiembesamaki Zanzibar baada ya kutangazwa mshindi.
  Mgombea wa Chama cha TADEA Mhe. Ali Mohammed Ali ameridhika na matokea hayo yaUchaguzi na ameridhika na kukiri hakuna Mamluki waliopita kupiga kura katika vituo hivyo na kusema waliopiga kura ni Wananchi wa Kiembesamaki tafauti na vyama vingine wanaolalamikia matokea hayo kuwa sio ya haki. Uchaguzi ulikuwa ni wa Huru na Haki.
  Mgombea wa Chama cha SAU Ramadhani Simai akizungumza na Waandishi wa habari na kumpongeza Mgombea wa CCM Mhe. Mahmuod Thabit Kombo kwa ushindi wake aliopata katika zoezi hilo la uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki na kuyapokea matokea hayo kwa mikonomiwili.
 Kiongozi wa Chama cha Siasa Zanzibar Mhe. Mshenga akielezea hali ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliokuwa ni wa Huru na Haki, hakuna mizengo iliofanyika katika Uchaguzi huo, Amesema amatembelea vituo vyote na kuridhika na hali ya upigaji kura kwa Wananchi wa jimbo hilo, Uchaguzi umekwenda kwa Amani bila ya vurugu hali hii ndiyo Ustaarabu wa Zanzibar kuwa na utulivu na amani wakati chaguzi. 
Viongozi wa Chama cha ADC,  wakibadilishana mawazo baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha Uwakilishi jimbo la Kiembesamaki wakijipongeza kwa ushindi walioupata wa kura 84 kwa mara ya kwanza kushiriki uchaguzi kwa Zanzibar na kujipa moyo watafanikiwa katika Chaguzin Kuu mwaka 2015. kutokana na matokeo hayo yanatia moyo kwa Chama chao.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.