Ads Top

MGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE KUPITIA CCM RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE AHANI MISIBA MIWILI

 Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiteta jambo  na kijana wa jamii wa wafugaji baada ya mkutano wake katika kijiji cha  Mkenge, kata ya Fukayosi
    Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Jana  katika Kijiji cha Mkenge, Kaya ya Fukayosi .
Mandhari kwenye mkutano wa kampeni za CCM Kijiji cha Kidomole, Kata ya Fukayosi jana
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akiwa kwenye msiba wa Zaidi muharami aliyefariki kwa ajali ya kugongwa na gari katika kata ya Fukayosi.


  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akiondoka kwenye msiba wa Zaidi Muharami aliyefariki kwa ajali ya kugongwa na gari.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akimpa mkono wa pole Mama Renata Paschal aliyefiwa na watoto wake wawili kwa ajali ya kuzama kisimani,aliyesimama pembeni ni Baba wa watoto hao ndugu Geofrey Nestroy.

 Ridhiwani Kikwete akitoa salaam za pole kwa familia hiyo ambayo imeondokewa na watoto wawili kwa pamoja katika kijiji cha Msinune kitongoji ya Kaloleni.
Makaburi ya Marehemu Redempta Geofrey aliyekuwa na umri wa miaka 2 na Jesca Geofrey aliyekuwa na umri wa miaka 5,wote walifariki kwa ajali ya maji baada ya kudumbukia kisimani tarehe 18 na kuzikwa tarehe 19 mwezi Machi katika kijiji cha Msinune kitongoji cha  Kaloleni.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.