Ads Top

TAARIFA:WATUHUMIWA 2 WAKAMATWA NA MENO 25 YA KIBOKO NA MMOJA AKAMATWWANA VIPANDE 8 VYA MENO YA TEMBO AMBAVYO NI NYARA ZA SERIKALI

Sehemu ya mali zilizokamatwa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova akionesha sehemu ya  vipande 8 vya meno ya tembo vilivyodakwa huko Tabata Kisiwani jijini Dar es salaam
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova akikagua gari linalotuhumiwa kutumika
 Jeshi la Polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata vipande zaidi ya ishirini (20) vinavyodhaniwa kuwa ni meno ya Tembo vilivyokuwa vimehifadhiwa nadni yamfuko maarufu kwa jina la kiroba. Tukio hili lilitokea tarehe 30/04/2014 katika kiwandacha Nondo Steel Master kilichopo eneo la Mbozi Road (W) kipolisi Chang’ombe (M) kipolisi Temeke baada ya Polisi kupokea taarifa kuwa katika kiwanda hicho kuna mfukowa kiroba wenye bidhaa hiyo umefichwa.
Baada ya taarifa hizo askari kikosi cha Upelelezi walifika kiwandani hapo na kwakushirikiana na Mkurugenzi wa Kiwanda hicho aitwaye HITESH S/O PATEL walifanyaupekuzi. Katika upekuzi huo, polisiwalifanikiwa kukamata vipande 25 vya meno yadhaniwayo kuwa ni ya KIBOKO vikiwa vimehifadhiwa ndani ya mfuko wa kirobaukiwa umefichwa kwenye Roll ambayo ni Malighafi maalum ya kutengenezea nondo. 
Kwa mujibu wa taarifa ya maafisa wa wanyamapori ni kwamba kwa idadi ya vipandehivyo 25 ni sawa na VIBOKO 6 waliouawa ambapo meno ya Kiboko mmoja yanathamani ya Dolla za Kimarekani 1500 sawa na Shilingi za Kitanzania zaidi ya (MillioniMbili Laki Nne na Sabini na Tano) Tshs.2,475,000. Hivyo kwa idadi ya VOBOKO sitathamani yake ni sawa na shilingi za Kitanzania THS; 14,850,000/= (million kumi nanne, mia nane na hamsini elfu tu).

Katika tukio hilo, polisi inawashikilia watu wawili ambao ni RASHID S/O ABDALLAH,Miaka 19, mwingine ni HEMED S/O JUMA @ KASIMU, Miaka 25. Washitakiwa haowatafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalowakabili pindi upelelezi utakapokamilika. 
Aidha katika tukio lingine mnamo tarehe 5/5/2014 huko maeneo ya Tabata Kisiwanikaribu na uwanja wa Twiga Mkoa wa Kipolisi Ilala, Polisi wamefanikiwa kumkamataMUSA S/O LUCAS KIFARU akiwa naa vipande 8 vya meno ya tembo vyenye uzito wakilogram 13.5 ambavyo thamani yake T.Shs.49,500,000/= vikiwa vimehifadhiwa kwenyebegi lenye rangi ya blue na nyeusi. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa .

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.