Ads Top

May 15 Kamata kamata bodaboda na bajaji mjini, Jiji lageuza biashara..!

 Tangazo lililobandikwa na Jiji kusitisha zoezi la ukusanyaji wa tozo/vibali vya kuingia mjini na pikipiki.
-Baadhi ya madereva wa pikipiki wanaozitumia kama vyombo vya usafiri binafsi kwenda na kurudi kazini wakihoji juu ya mkanganyiko huo katika ofisi za Jiji la Dar es Salaam, juzi. Hata hivyo hawakupata majibu zaidi ya kukuta tangazo lililositisha upokeaji wa toza za kuingia mjini na vibali.
ZOEZI la kupiga marufuku bodaboda na bajaji zinazofanya biashara katikati ya Jiji la Dar es Salaam limegeuka biashara kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam hasa kwa watumiaji wa pikipiki hizo kwa ajili ya usafiri binafsi wa kawaida kwenda na kurudi kazini, pamoja na makampuni yanayotumia chombo hicho cha usafiri.

Halmashauri ya jiji sasa imeanza kuwatoza watu binafsi na makampuni yanayotumia chombo hicho shilingi 500 kwa siku kila bodaboda inapoingia mjini wakidai ni tozo ya chombo hicho kupata idhini ya kuingia mjini kwa kila siku.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.