KUTOKA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA NCHINI: SHEREHE ZA KUAGA WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA MKOANI MWANZA

Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoani Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Magereza Mstaafu, Raphael Mollel akitoa nasaha zake kwa niaba ya
Wastaafu wote wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza katika sherehe za
kuwaaga Wastaafu wa Magereza Mkoani Mwanza.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa
hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza na Wageni Waalikwa (hawapo
pichani) katika Sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani
Mwanza.

Wageni Waalikwa katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza
Mkoani Mwanza wakitosi vinywaji na Meza Kuu kama inavyoonekana katika
picha.

Meza Kuu katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani
Mwanza (katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John
Casmir Minja ambaye pia ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo
zilizofana katika Ukumbi wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza.

Maafisa na Askari wa Magereza Mkoani Mwanza wakimsikiliza Mgeni rasmi
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati
akitoa hotuba yake fupi katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la
Magereza Mkoani Mwanza katika Ukumbi wa Bwalo la Gereza Kuu Butimba,
Jijini Mwanza.
No comments: