WASHIRIKI 20 WA SHINDANO LA TMT WAINGIA RASMI KAMBINI JANA USIKU, TAYARI KWA SAFARI YA KUWANIA MILIONI 50
Muonekano
wa TMT House ambayo washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents
wameweka kambi rasmi kuanzia jana Usiku kwa mchakato wa kuwania Milioni
50 katika fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane
Mmoja
kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kusini, Mwanaafa Mwizago
akiingia rasmi kambini hapo jana wakati wakitokea kwenye matembezi.
Washiriki wote 20 ambao ni washindi kutoka Kanda sita za Tanzania sasa
wapo kambini kwaajili ya kujifua ili kuwania kitita cha Shilingi Milioni
50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane.
Baadhi ya washiriki wa Fainali ya Shindano la TMT wakiingia kambini hapo jana Usiku
Washiriki wakipewa maelekezo mara baada ya kuwasili kambini hapo jana
Washiriki
20 kutoka Kanda sita za Tanzania wameingia rasmi kambini hapo Jana mara
baada ya kumaliza zoezi la Kupima Afya, kutembezwa sehemu mbalimbali za
Jiji la Dar pamoja na Ofisi za Global Publishers.
Washiriki
hao watakaa kambini kwa Siku 64 ambapo wataanza rasmi kufundishwa Hapo
kesho siku ya Jumatatu na walimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na
Chuo Cha Sanaa Bagamoyo ambapo baadae sasa baadae zoezi la kuanza
kuwapigia kura washiriki hao litaanza na hatimaye watanzania ndio
watakuwa majaji kwa washiriki hao ambapo mshindi mmoja wa Shilingi
Milioni 50 atapatikana katika Fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi
wa Nane.
Zoezi
la Upigaji kura litaanza mapema wiki ijayo ambapo washiriki wote
watakuwa tayari washapewa namba za ushiriki na hatimaye watanzania
kuweza kuwachagua washiriki wanaowaona wana vipaji.
Zoezi
hili la kupiga kura litapelekea Washiriki wawili kuondolewa kila wiki
katika Kambi ya TMT ambapo pona yao ni kutoka kwa Watanzania ambao ndio
watakuwa majaji kwa kuwapigia kura.
Vilevile
Mara baada ya washindi hawa wa kanda kuingia kambini Vipindi vyetu
vitaendelea Kurushwa kila siku ya Jumamosi Saa 4 Usiku na Kurudiwa kila
Siku ya Jumapili Saa 10 Jioni na Jumatano Saa tano usiku kupitia Runinga
ya ITV.
Tunawaomba
watanzania kuendelea kutizama vipindi vyetu kwani vimekuwa na mvuto wa
hali ya juu sana lakini pia kuendelea kuwawezesha Washiriki wanaowaona
wana vipaji ili kuwa ushindi.
Namba
za washiriki zitaanza kuonekana katika Kipindi chetu kijacho ambapo
Sasa watanzania wataanza kuwapigia kura kwenda namba 15678Na ili kuweza
Kufahamu taarifa zaidi za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba
15678.
No comments: