Timu ya taifa ya soka ya Ujerumani imewasili nchini humo kwa kishindo wakiwa na kombe lao la ushindi walilolinyakua katika mashindano ya kombe la dunia ambyo yalikamilika juzi nchini Brazil.
Timu ya taifa ya soka ya
Ujerumani imewasili nchini humo kwa kishindo wakiwa na kombe lao la
ushindi walilolinyakua katika mashindano ya kombe la dunia ambyo
yalikamilika juzi nchini Brazil.
Maelfu ya mashabiki wa soka wamekuwa wakisubiri tangu asubuhi na mapema mjini Berlin kuwakaribisha wachezaji hao.
Sherehe zitafanyika katika eneo la
Brandenburg Gate, ambako wachezaji wataonyeshea kombe lao, ambalo
walilishinda katika fainali ya mashindano hayo dhidi ya Argentina.
Shangwe na vigelegele vimeshuhudiwa huku umati mkubwa wa watu ukitarajiwa kushuhudia kombe hilo ambalo litapitishwa mjini kote.
Watu wengi wamenunua jesi zenye nyota nne kuashiria ushindi wa nne wa nchi hiyo katika kombe la dunia.
Wachezaji wa timu hiyo ambao huchezea timu ya Bayern Munich pia watapata ukaribisho mkubwa baadaye mjni Munich.
Watu wengi wamenunua jesi zenye nyota nne kuashiria ushindi wa nne wa nchi hiyo katika kombe la dunia.
No comments: