Marekani imeanzisha mfululizo wa mashambulizi mapya ya anga huko Syria kwa ushirikiano na nchi tano za Kiaraab zinazounga mkono mapambano dhidi kundi la IS
Kamanda wa Marekani anasema tayari wamefanikiwa kuangamiza kituo cha
mafunzo cha wapiganaji wa dola ya Kiislam,vifaa na magari yao huko
kaskazini na Mashariki mwa Syria.
Taarifa zinasema kuwa mashambulizi hayo yanalenga mji wa Raqqa ambako ni makao makuu ya wapiganaji hao.
Uingereza
imesema kuwa baadhi ya wapiganaji wa kundi hilo wameuawa. Hata hivyo
mashambulizi yamelenga mtandao wa Al Qaeda ambao unadaiwa kushirikiana
na wapiganaji wa kundi la kiislam ambalo limekuwa likiwalenga raia wa
Mgahribi.
Habari na BBCswahili,com
No comments: