Ads Top

Wakala wa huduma za ajira Tanzania (TaESA) wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa watafuta kazi 2146 katika harakati za kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri hapa nchini.

Afisa Habari wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) Bi. Jamila Mbaruku akiewaeleza waandishi wa Habari( hawapo pichani) kuhusu kuhusu mikakati ya wakala wa huduma za ajira kusaidia wananchi wa tanzania kuingia katika ushindani wa soko la ajira nchini ikiwemo kutoa mafunzo kwa Watafuta kazi.Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Tawala wa Wakala hiyo Bw. Peter Ugata.
Afisa Tawala wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) Bw. Peter Ugata akitoa wito kwa wadau na wananchi kwa ujumla kutumia wakala huu unaowaunganisha waajiri na watafuta kazi nchini.wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Afisa Habari wa Wakala huo Bi. Jamila Mbaruku.



Wakala wa huduma za ajira Tanzania (TaESA) wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa watafuta kazi 2146  katika harakati za kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri hapa nchini.




Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Afisa Habari wa Wakala huo Bi Jamilah Mbarouk wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.



Akifafanua Bi Jamilah amesema kati watafuta kazi waliopatiwa mafunzo hayo wanaume ni 1254 na wanawake ni 879.


“Vile vile wakala umeweza kutoa mafunzo haya kwa vyuo vitano (5) ambavyo ni Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM), Taasisi ya Uhasibu (TIA),Chuo cha ardhi na Taasisi ya ya Teknolojia Dar es salam ambapo vyuo vyote viko Dar es salaam na kushirikisha wanavyuo 860.”alisema Jamilah Kwa sasa mafunzo haya hutolewa kila ijumaa kwa watafuta kazi waliosajiliwa TaESA.





Katika kutoa mafunzo  hayo TaESA imelenga kuwajengea uwezo watafuta kazi kuwajengea uwezo na ujuzi wa kuandika barua za maombi  ya kazi,jinsi ya kufanya usaili kwa kujiamini na kuelewa kuhusu matarajio ya waajiri kwa wafanyakazi.



Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaEsa) ulianzishwa kwa sheria ya wakala Na. 30 ya mwaka 1997 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2009) na kuzinduliwa rasmi tarehe 16 june,2008 kufuatia tamko la Serikali Na.189 la mwaka 2008 na kuanza shughuli zake tarehe I julai,2008 ikichukua nafasi ya kilichokuwa kituo cha ajira nchini (Labour Exchange Centre).

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.