Kisa cha kushangaza kilitokea nchini Nigeria ambapo mwanamke mmoja alipewa kichapo kikali hadi akafariki kwa madai ya yeye kuwa mchawi
Mwanamke huyo inasemekana alikuwa Ndege iliyokuwa inaruka mtini kabla ya kugeuka na kuwa binadamu.
Umati
wa watu ulikusanyika eneo alilokuwa mwanamke huyo baahi wakinasa
matukio kwenye simu zao za mkononi. Polisi wawili walilazimika kurusha
mabomu ya petroli kuwatawanya watu hao na kuwazuia kunasa picha za
mwanamke huyo aliyekuwa anachapwa sana.
Kwa mujibu wa
walioshuhudia, mmoja alisema kuwa mwanamke huyo dakika chache zilizopita
alikuwa Ndege mtini kabla ya kugeuka na kuwa mwanamke.
Ndege huyo
alikuwa anazunguka mti mjini Oshodi , kisha akagonga mlingoti wa stima
kabla ya kuanguka ardhini ambapo aligeuka na kuwa mwanamke.
Hii ni kwa mujibu wa wakazi wa mjini Oshodi wanaodai kuwa mwanamke huyo alikuwa mchawi.
'Kitu cha kushangaza'
''Ni kitu cha kushangaza lakini ni cha kweli,'' alisema bwana Sobowale.
"tulipozungumza
na mwanamke huyo alidai kuwa na nguvu za kiganga, na kwamba alikuwa
amewaua watu kadhaa. Aliongeza kuwa alikuwa anarejea kwa mumewe
anayeishi katika eneo la Mushin kabla ya tyukio hilo. Baadhi ya watu
walianza kumpiga picha. ''
Video ya umati huo ukimtandika mwanamke
huyo imeenea kama moto msituni na kutazamwa na maelfu ya watu kwenye
mtandao wa kijamii wa YouTube.
Mwanamke huyo alikuwa uchi wa mnyama huku ngozi yake ikiwa inatoka baada ya kuchomwa.
Banke
Idowu ni mmoja wa watu walionasa video ya mwanamke huyo akiwa anachapwa
na umati na kwamba alikuwa amearifiwa na wenzake kuhusu mwanamke huyo
alivyobadilika.
Aliambia BBC kuwa "sijawahi kuona jambo kama hili
maishani mwangu,lakini nimesikia na kuona tu kwenye filamu kwa hivyo
waliponiambia kuwa limetokea , mimi nimeamini. ''
Alisema angedhubutu kumuokoa mwanamke huyo umati huo ungemgeukia na yeye.
Polisi hawajuzungumzia tukio hilo, hususan kabla ya umati huo kukusanyika na kuanza kumchapa mwanamke huyo.
Alifariki mda mfupi baadaye huku mwili wake ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu.
No comments: