WAZIRI MUHONGO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA MCC
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisistiza
jambo katika kikao baina ya Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za
Millenia (MCC) Kamran Khan (wa pili kushoto) na ujumbe wake akiwemo
Balozi wa Marekani nchini Mark Childress(wa kwanza kushoto). Wengine wa
kwanza ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
Ngosi Mwihava na watendaji wa Wizara,na wa taasisi za Wizara
wakifuatilia kikao hicho
Makamu
wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan ( wa
kwanza kushoto ) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) anayesikiliza katikati ni Balozi wa
Marekani nchini, Mark Childress mara baada ya kikao hicho.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo katikati) katika picha ya
pamoja ofisini kwake na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za
Millenia (MCC) Kamran Khan (kushoto) na Balozi wa Marekani nchini , Mark
Childress (Kulia)..
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan na Ujumbe wake akiwemo Balozi wa Marekani nchini Mark Childress, katika kikao kilicholenga kujadili maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa MCC Awamu ya pili na masuala ya kuendeleza sekta ya nishati nchini.

Kikao
hicho kimezihusisha pia taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na
Madini ikiwemo, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi
Tanzania (TGDC) pamoja na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Shirika
la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na
Nishati (EWURA).
Katika
kikao hicho, Profesa Sospeter Muhongo amezitaka taasisi hizo kutekeleza
miradi hiyo kwa kasi zikizingatia suala la uwajibikaji, ubunifu, uwazi
na kuongeza kuwa, miradi hiyo itatekelezwa bila kuwepo na mazingira ya
rushwa , huku akisisitiza ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi
katika uendelezaji wa miradi hiyo.
Kwa
upande wake Makamu wa Rais wa MCC, Kamran Khan ameahidi kutoa
ushirikiano kwa Wizara katika kutekeleza miradi hiyo ambayo inalenga
kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Mark Childress amesisitiza suala la kuzingatia muda katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuongeza kuwa, hakuna sababu itakayokwamisha miradi hiyo.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Mark Childress amesisitiza suala la kuzingatia muda katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuongeza kuwa, hakuna sababu itakayokwamisha miradi hiyo.
No comments: