BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YAJIPANGA KUTATUA KERO ZA WANAFUNZI.

Bodi
ya mikopo ya elimu ya juu nchini imesema kwasasa imekwishaimarisha
mifumo yake ya kupokea na kushuhulikia malalamiko ya wanafunzi haswa kwa
waliokosa mikopo kwenye bodi hiyo.
Hayo yamebainiswa na meneja wa habari, elimu na mawasiliano wa bodi
hiyo Bwana Omega Ngole huku akisema bodi hiyo kwasasa imejipanga vyema
katika kuhakikisha wanafunzi wanaomba mikopo wanapata mikopo kwa wakati.
Bwana Omega Ngole ametoa wito kwa mafisa mikopo wa vyuo hapa nchini
kuhakikisha wanabainisha matatizo ya wanavyuo na kuyashuhulikia kwa
wakati ili kupunguza migogoro ya wanavyuo hao katika upatikanaji wa
mikopo.
No comments: