SERIKALI YAWATAKA WATENDAJI TRA KUACHA KUWATISHA WAFANYABIASHARA MKOANI KILIMANJARO.

Waziri
wa fedha na mipango Mh Dr. Philp Mpango amesema hakuna mtendaji wa
serikali aliyejinufaisha na mapato ya serikali atakaye samehewa na
hakuna mtendaji mwadilifu atakayeonewa.
Mh .Dr Mpango ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na watendaji wa kituo cha pamoja cha forodha cha Holili mkoani Kilimanjaro.
Aidha amewataka maafisa wa TRA kukufanyakazi kwa uadilifu na kuacha
kutumia kampeni zinazoendelea za kudhibiti mapato kuwatisha
wafanyabiashara badala yake wawasaidie waweze kuzalisha na kulipa kodi
halali.
Aidha amewataka watendaji wa mamlaka ya mapato ambao bado
hawajatangaza mali zao wanazomiliki kufanya hivyo mara moja kwani hakuna
njia ya mkato lazima lengo la serikali la kuisafisha mamlaka hiyo mbele
ya jamii litimie.
Kuhusu malalamiko ya kuendelea kuwepo kwa usumbufu wa baadhi ya
watendaji wanaotumia nyadhifa zao kuwasumbua na wasafirishaji wa bidhaa
na kuwawekea vikwazo barabarani Dr Mpango amesema siku zao zinahesabika
na amewataka wananchi na watumishi wadilifu kuwafichua kwani
wanawasababishia watu wengine matatizo.
Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro Bw Abdul Mapembe amesema
ukusanyaji wa mapato unaendeleabkuongezeka siku hadi siku licha ya
kuwepo kwa baadhi ya changamoto ikiwemo ya uhaba wa vitendea kazi.
Kwa sasa ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka bilion mia tisa hadi kufikia trilion 1.6 kwa mwezi.
No comments: