JESHI LA POLISI LAUA MAJAMBAZI WATATU KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI MKOANI ARUSHA.

Jeshi
la Polisi mkoa wa Arusha limewaua kwa risasi watu watatu wanaodaiwa
kuwa ni majambazi na kukutwa na bunduki moja aina ya AK 47 ikiwa na
risasi kumi na nane milipuko ishirini na saba sale za jeshi la wananchi
wa Tanzania na bendera inayodaiwa kutumiwa na kikundi cha Al Shababy
katika tukio lililotokea eneo la Engosheraton Sinoni jijini Arusha.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Libaratus Sabas amesema
jeshi la polisi lilipata taarifa ya uwepo wa majambazi hao kutoka kwa
wasamariawema wakitaka kufanya tukio na baada ya kufika katika eneo la
tukio watu hao walianza kurusha risasi kwa askari lakini askari
waliwashinda nguvu na kufanikiwa kuuwa majambazi watatu ambapo mmoja
akifaamika kwa jina la Athumani Ramadhani.
Aidha kamanda Sabas amevitaja vifaa pamoja silaa zingine walizi
kutwa nazo majambazi hao ikiwa ni pamoja na pikipiki simu na vingine
mapanga na visu kama anavyoeleza na baadhi ya wananchi wakilitaka jeshi
la polisi kuendelea kuzibiti ongezeko la silaa na kuchunguza mahali
panapo toka silaa hizo za kijeshi ambazo zimeenea katika maeneo mengi ya
raia.
No comments: