DAKTARI ASIMAMISHWA KAZI KWA KUOMBA RUSHWA KWA MGONJWA LAKI MOJA MTWARA.

Waziri mkuu mh Kassimu Majaliwa amelazimika kutembelea hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Ligula na kujionea madudu baada ya kuombwa na wananchi
akiwa katika mkutano wa hadhara na kufanikiwa kumsimamisha kazi Dokta
Fortunatus Namahala aliyeomba rushwa ya shilingi laki moja kutoka kwa
mgonjwa.
Alipowasili katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ligula Mh Majaliwa
akakumbana na kundi kubwa la wananchi na wakawa na haya ya kumueleza.
Mh Majaliwa mara baada ya kutembelea hospitali hiyo na kupata
malalamiko kutoka kwa wananchi akalazimika kuitisha kikao cha dharura
cha madaktari pamoja na watendaji wa hosptali hiyo baada ya kuonyesha
kukerwa na malalamiko ya wananchi dhidi ya madaktari.
Hata hivyo baada ya daktari aliyeomba rushwa kubainishwa na muhusika Mh waziri mkuu akawa na ujumbe huu.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Dokta Hindi Mastai akalazimika
kumweleza waziri mkuu pamoja na lawama nyingi kwenda kwa madaktari
mazingira wanayofanyia kazi ni haya.
No comments: