MKE WA RAIS AWAAHIDI WALIMU NCHINI KUMKUMBUSHA RAIS MATATIZO YAO.



Mke wa rais Mama Janeth Magufuli amewaahidi walimu nchini kuwa atahakikisha anamkumbusha rais changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo walimu ili ziweze kutatuliwa kwa wakati kwani anazifahamu na amezipitia.
Mama Janeth ametoa ahadi hiyo jijini Dar es Salaam alipokwenda kuwaaga wanafunzi na walimu wa shule ya Mbuyuni ambayo mbali na kufundisha kwa miaka 17 lakini pia alikuwa mwanafunzi wa shule hiyo ambapo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wazazi na walezi nchini kutosahau majukumu yao kisa dhana ya elimu bure.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi Doroth Malechela akatumia ipasavyo
ujio wa mke wa rais kumuomba afikishe kilio cha walimu nchini kwani
wanakabiliwa na matatizo lukuki ikiwemo mazingira magumu ya kazi, fedha
za likizo kutokupatikana kwa wakati kutopanda madaraja kwa wakati na
wakipanda upatikanaji wa stahiki zao imekuwa matatizo.
Katika risala yao wanafunzi wa shule ya msingi Mbuyuni mbali na
kumweleza mke huyo wa rais mapungufu yaliyojitokeza pindi tu alipoondoka
wamemuomba asiwasahau kama wanavyoeleza.
Tanzanian Shilling Converter
No comments: