WAKAZI ZAIDI YA 150 GONGOLAMBOTO WATALAZIMIKA KULALA NJE BAADA YA NYUMBA ZAO KUBOMOLEWA.


Wakazi zaidi 150 wa Guluka kwalala Gongolamboto jijini Dar es Salaam
ambao nyumba zao 25 zimebolewa wamesema kwa sasa watalazimika kulala nje
kwa kukosa nyumba za kuishi baada ya zoezo la bomoabomoa kufanywa na
uongozi wa kiwanda cha kampuni ya NAMERA huku wakazi hao wakisema zoezi
zima la ubomoaji limefanyika wakati kesi kuendelea kusikilizwa katika
mahakama ya ardhi.
Wakiongea na ITV mara baada ya kufika katika eneo hilo la Guluka
kwalala na kushuhudia mabaki ya nyumba ambazo zimebomolewa wananchi hao
wamelalamikia zoezi zima la ubomoaji wa nyumba hizo baada ya idadi kubwa
ya wakazo hao kushindwa kutoa samani zao ndani wakati zoezi la ubomoaji
likifanyika na kusimamiwa na askari wa jeshi la polisi.
Bwana Fitiri Juma ambaye ni mjumbe wa seikali ya mtaa wa Guluka
Kwalala akiongea na ITV amelalamikia viongozi wote wa eneo hilo kutofika
wakati zoezi la ubomoaji likendelea na kusababisha wananchi hao kupata
hasara ya mali zao.
Katika kutaka kujua juu ya uhalali wa zoezi zima la ubomoaji kama
limezingatia misingi ya sheria ITV iliutafuta uongozi wa kiwanda cha
NAMERA ambapo uongozi umekiri kutelezela zoezi hilo na kulipa fidia
wananchi wote waliojenga eneo hilo wanalodai ni la kiwanda.
Chanzo ITV
Tanzanian Shilling Converter
No comments: